Tume ya Ukimwi Pemba
yakabidhiwa gari
29/01/2010

Katika Kile kilichoonekana kuwa ni moja
wapo ya hatua za kuendeleza mbele mapambano ya vita dhidi ya maambukizi
mapya ya virusi vya Ukimwi, Katibu Mkuu Afisi ya Waziri Kiongozi Msham
Abdallah Khamis, amekabidhi gari kwa Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba Nd.
Nassor Ali Abdallah kwa ajili ya kufanyia ufuatiliaji na uratibu wa
shughuli mbali mbali za ukimwi kisiwani Pemba.

Kushoto ni Mkurugenzi wa Tume ya Ukimwi
Zanzibar, Bi Asha Abdallah. Msaada wa gari hilo ni kutoka katika Benki
ya Dunia.
|