Jerry Muro kizimbani
05/02/2010

Mtangazaji wa TBC Jerry
Muro akisindikizwa kuelekea chemba kusomewa mashitaka ya kula njama ya
kutaka kupokea rushwa ya shilingi milioni 10 leo mahakama ya hakimu
mkazi kisutu jijini Dar es Salaam.

Jerry Muro chini ya ulinzi
mkali mahakamani.

Waandhishi wa habari mbalimbali walikuwapo
katika mahakama hiyo akiwamo kaka Michuzi (pili kushoto).

Jerry Muro akiingia ndani ya gari yake
huku akipooza koo baada ya kuachiwa kwa dhamana.

Mshtakiwa mwenza na Jerry
Muro, Edmund Kapama, akiondoka kwa furaha mahakamani baada ya kuachiwa
kwa dhamana leo.
HABARI KAMILI:
Mtangazaji wa TBC Jerry Muro na watu wengine wawili, Edmund Kapama na
Deogratius Ngassa, wamepanda kizimbani mchana huu wakikabiliwa na
mashataka kadhaa likiwemo la kula njama kutaka kupokea rushwa.
Mbele ya
Hakimu Gabriel Mirumbe, Jerry Muro na washtakiwa hao wawili walishtakiwa
kwa pamoja kwa kuomba rushwa ya shilingi milioni 10 toka kwa mweka
hazina wa wilaya ya Bagamoyo aliefukuzwa kazi hivi karibuni na Waziri
Mkuu kwa ubadhirifu Bw. Michael Wage.
Mwendesha Mashtaka wa Serikali Boniface Stancilaus akiwa na Mwendesha
Mashtaka toka TAKUKURU Benny Lincolin wamedai mahakamani hapo kwamba
mshtakiwa wa kwanza na wa pili pia wanakabiliwa na shtaka la kujipachika
wadhifa ambao sio wao.
Inasemekana January 29, 2010 katika hoteli ya Sea Cliff washtakiwa
walijitambulisha mbele ya Wage kuwa wao ni maafisa wa Takukuru wakati
sio kweli.
Upande
wa mashtaka uliiomba mahakama usitoe dhamana hasa kwa washtakiwa wa
kwanza na wa pili kwa madai kwamba waliwahi kufungwa huko nyuma na kuwa
kwao nje kutaharibu upelelezi ambao haujakamilika na bado unaendelea.
Hakimu
alipowataka kutoa uthibitisho kwamba washtakiwa hao waliwahi kufungwa
huko nyuma upande wa mashtaka ulishindwa kuthibitisha hivyo dhamana
ikawa wazi kwa m ashartia ya kila mmoja kuwa na wadhamini wawili
wataosaini bondi ya milioni 5 kila mmoja, ama kwenda rumande hadi
Februari 12, mwaka huu kesi itaposomwa tena.
Jerry Muro na Edmund Kapama walitimiza
masharti ya dhamana na kuachiwa. Mwenza Ngassa amepelekwa rumande.

Madai ya Jerry Muro na wenzake.
|