Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Matokeo ya kidato cha nne (Form 4)

06/02/2010

Hongera kwa wote waliopiga hatua kimasomo na kumaliza elimu ya kidato cha nne mwaka 2009.

Unaweza kutizama matokeo ya mtihani wa Taifa kuhitimu katika ngazi hiyo ya elimu kwa njia mbili. Moja ni kwa kutumia tovuti na nyingine ni kwa kutumia simu kwa wateja wa VodaCom pekee.

Bonyeza kujaribu kati ya linki zifuatazo:
  1. www.tetea.org/olevel.htm
  2. www.moe.go.tz/NectaResults/olevel.htm
  3. www.necta.go.tz/html_csee209/olevel.htm
  4. www.necta.go.tz/publishedresults/csee.php
AU
Tumia simu ya mteja wa VodaCom.
Tuma ujumbe mfupi wa maneno (sms) kwenda 15311 yenye message: MatokeoXcentreXcandno
Badili neno 'centre' na uandike jina la shule/kituo ulichofanyia mtihani
Badili neno 'candno' na uandike namba ya mtahiniwa
Kwa mfano: MatokeoXS0452X0203
Shukrani zimwendee Augsustine Maguta aliyetushirikisha njia mbadala.

ANGALIZO:
Ikiwa namba ya kituo ulichofanyia mtihani namba zake zina tarakimu chini ya nne, unahitaji kubandika tu tarakimu hizo bila kutanguliza sifuri.
Kwa mfano: Namba ya shule/kituo ni S0012 na namba ya mtahiniwa ni 45 basi andika MatokeoXS12X45

Huduma zilizotajwa hapo juu kwa ajili ya matokeo haya hazitatozwa fedha yoyote ile.

ILANI:
Tovuti ya matokeo inaweza kutokuwa hewani (off line due to bandwidth limit) kutokana na kuzidiwa na wingi wa watu wanaotaka kuona matokeo. Hilo ni suala la IT wanaohusika na wizara hiyo wanaweza kulirekebisha. Ufikwapo na hali hiyo, pole kwa usumbufu huo, ndivyo Wizara zetu za Serikali zilivyo na bandwidth ndogo il hali uhitaji ni mkubwa, hasa kwa tovuti hii ambayo imekuwa ikilalamikiwa kwa miaka mitatu mfululizo kwa tatizo hili hili, sifahamu mkakati wao wa kulitatua tatizo hili.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007