Mtanange wa Simba na Yanga
ughaibuni kufanyika Aprili 4
09/02/2010

Yanga
Mechi ya
kwanza ya Simba na Yanga mwaka huu itafanyika Jumapili April 4, kwenye
uwanja wa Kalmia, kufuatia mechi itakayochezwa Jumamosi kati ya Stars
united na Maryland united japo uwanja itakapochezwa mechi hiyo bado
kutangazwa.
Mtayarishaji wa mpambano huo wa Stars na Maryland United, Cyprian,
amesema kutakua na nyama choma siku hiyo ya Jumamosi April 3, na mechi
hii ni re-union ya wachezaji wote wa Maryland United na kutakuwa na
zawadi maalum kwa wachezaji wa zamani wa timu hiyo.
Wachezaji Watanzania waliowahi kuichezea Maryland united ni Liberatus,
Mwang'ombe, Vicent Ndusilo, Chiwa Mwombela, Elvis Dotto na Yahaya Kheri.
Cyprian ameiomba Stars united wachezaji hao wachezee Maryland united
siku hiyo ya mpambano.
Salum Salum amesema yeye hana mkwara wowote, wachezaji hao wanaweza
kuchezea timu hiyo, lakini wajue hawatakiwi kuifunga timu yao, mchezaji
yeyote atakaeifunga timu yake ya Stars United ajue amefungiwa, wewe
cheza tu lakini ujue unatoa pasi tu.

Simba
|