Gari yaacha barabara na
kupanda mti
11/02/2010

Gari lenye namba za usajili T 857 BAR,
likiwa limening’inia juu ya mti katika daraja la Kawe lililopo Mbezi kwa
Komba, Dar es Salaam.

Haikuweza kufahamika chanzo cha ajali ya
gari hilo, kwa mujibu wa walioshuhudia ajali hiyo walieleza kuwa ajali
hiyo ilitokea saa tisa usiku.

Huu ni upande wa chini ya gari hilo
linavyoonekana likiwa juu ya mti, ambapo imeelezwa magari kadhaa
yalifika kutoa huduma ya kuliondoa mahala hapo bila mafanikio.

Askari wa usalama barabarani, akiongoza
magari ili kuondoa foleni ambayo ilikuwa ikisababishwa na madereva
waliokuwa wakishangaa ajali hiyo jambo ambalo lilifanya kila dereva
kupunguza mwendo afikapo eneo hilo.
|