![]() |
|
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS |
||||||||
|
|
||||||||
Stay Tuned, I'll be back in June13/02/2010
KIPINDI cha TV cha The Apprentice UK kawaida huonyeshwa kila mwezi wa tatu (Machi) kila mwaka katika kanati (channel) ya TV ya BBC London. Kipindi ambacho huchagua mfanyakazi bora baada ya kupitia wiki takriban 12 katika washindani 12 au 13 ambao wanagombea nafasi moja ya kuwa The Apprentice wa kufanya kazi katika kampuni mojawapo ya makampuni ya bosi wa kipindi hicho Sir Alan Sugar kwa mshahara usiopungua £100,000 kwa mwaka. Kipindi hicho mwaka huu kimehairishwa badala ya kurushwa hewani mwezi Machi 2010, kitarushwa hewani mwezi Juni 2010 kwenye kanati ya BBC kwa kinachosemekana kuwa kipindi hicho kifanyike baada ya uchaguzi mkuu wa kitaifa wa UK wa mwaka 2010 ambao unatarajiwa kufanyika mwezi Mei 2010. Bwana Alan Sugar alipoulizwa na waandishi wa habari wa gazeti la "The Mirror" maoni yake kuhusu kuhairishwa kwa kipindi hichi mpaka Juni 2010 badala ya kuwa Machi 2010 alisema, “They’ve delayed it for some political reason which is a bit of a joke in my opinion." Sir Alan Sugar hivi karibuni (2009) amechaguliwa na serikali kuwa mmoja wa mabwana "Lords" katika kuchangia fikra za kiuchumi nchini UK. Mwaka jana mmoja wa aliyeshiriki katika mashindano ya kufanya kazi na Sir Alan Sugar alikuwa ni Mtanzania MONA LEWIS. Kwa habari zaidi za Mon Lewis bonyeza hapa.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||