Mnara wa msikiti waanguka
Morocco
20/02/2010

Wafanyakazi wa huduma za uokoaji katika
mji wa Meknes nchini Morocco wamekuwa wakiendelea na utafutaji wa
manusura kufuatia kuanguka kwa mnara wakati wa swala ya Ijumaa. Kwa
uchache watu thelathini na sita waliuwawa na wengine zaidi ya sabini
walijeruhiwa.
Inaarifiwa kuwa watu wengine zaidi
wamefukiwa chini ya kifusi cha mnara huo. Baadhi ya waokoaji wamekuwa
wakijaribu kuwafikia manusura wakitumia mikono yao kwa sababu mashine
kubwa na nzito haziwezi kupita kwenye barabara finyu za mji huo wa kale.
Maafisa walisema siku kadhaa za mvua kali
ziliathiri mnara huo uliojengwa karne kadhaa zilizopita katika mji wa
kihistoria wa Meknes.
|