Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

TANZANIA DIASPORA 2: London 26th - 27th March yafana

26/03/2010

Kongamano la pili la Watanzania wanaoishi UK limefana kikamilifu leo hii kwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa jumuia za Watanzania wanaoishi UK, uongozi wa ubalozi wa Tanzania UK, na, mashirika na viongozi mbalimbali wa taifa letu akiwamo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe.

Serikali ya Tanzania imejikita na kutilia mkazo kwa umuhimu wa mkutano huu wa 'Diaspora UK' kwa kuwaletea mafanikio Watanzania wanaoishi UK ili waweze kufaidika na nyumbani Tanzania kwa maendeleo yao wenyewe na maendeleo ya taifa lao kwa kuashiria kuwa Watanzania walio nje ya nchi pamoja na Vizazi vyao hawajasahauliwa na viongozi wao na wala nchi yao haijawatupa na huo ndio ujumbe aliokuja nao Mh. Bernard Membe kwa Watanzania wanaoishi UK kutoka kwa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete.

Kwanini UK tu kwa sasa? Kwasababu UK ndio nchi ya kwanza kuanzishwa kwa 'Diaspora Association' kwa jitihada na ari za Viongozi wa jumuia za Kitanzania zilizopo UK na kuvaliwa njuga na Balozi wetu Mwanaidi Maajar ambaye alilisimamia na kulihimiza hili jambo bila ya kuchoka.

Aidha, ni shauku kubwa vilevile ya Rais wetu Kikwete kuona hili jambo linatekelezwa ipasavyo si tu kwa faida ya Watanzania wanaoishi UK, bali ni kwa Watanzania wote wanaoishi ughaibuni kama alivosema kwenye barua yake ya wazi kwa Watanzania wanaoishi UK kuwa, "Whenever I met Tanzanians living abroad, I never hesitated to remind them of this important and historic duty of theirs." Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Yote hayo yalielezwa kwa ufasaha na kwa undani kabisa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mh. Bernard Membe, kuwa vipi serikali yake imejikita na suala hili na nini manufaa yake kwa Watanzania wanaoishi UK na ughaibuni kwa ujumla na manufaa ya taifa.

Manufaa ya Taifa:

Katika hotuba yake ya kihistoria ya takriban dakika 40, Mh. Membe alisema kwa kutoa mfano nchi za jirani vipi zinafaidika na Wananchi wao wanaoishi nchi za nje kuwa zinaingiza mabilioni ya pesa kutoka kwa wananchi wao wanaoishi nje ya nchi kwa kuwapatia mfumo maalum ambao unawasaidia kuwekeza nyumbani katika njia mbalimbali na kuendeleza hali ya kiuchumi nchini kwao, na ndio mfumo huo umetiliwa mkazo na serikali ili isaidie Watanzania walio nje ili kujenga nchi yao.

Manufaa ya Kila Mtanzania anayeishi UK (Ughaibuni):

Mh. Membe amesema, tumefika hapa na mashirika mbalimbali ya nyumbani Tanzania kuwapatia fursa Watanzania wanaoishi hapa UK kwenye maeneo ya Ajira (kazi) ili kuwafaidisha Watanzania wanaopendelea kurudi nyumbani kwa kuleta maendeleo ya kiuchumi. Alisema yote haya yameandaliwa na kuwekwa mezani na serikali kwa kuwafaidisha Watanzania, iliyobaki ni Watanzania wajitokeze inapotokea fursa hizi ili wazichukue kwa manufaa yao na nchi yao.

Mh. Membe alisisitiza na aliwaomba Watanzania wa Ughaibuni mambo ya Kisiasa wawaachie Wanasiasa, lakini hili ni jambo la kila Mtanzania.

Katika mambo ya Uhamiaji, Mh. Membe amesema, ubalozi wa UK utakuwepo kwa mpangilio maalum kusikiliza na kutoa ushauri kwa Watanzania wanaoishi UK, na alisisitiza Watanzania kushiriki katika vyama vyao katika ngazi ya mkoa ili yale mahitaji yao binafsi yapelekwe katika ngazi ya kitaifa ya Diaspora Association (TZUK) na kuwakilishwa serikalini ili kuyafanyia kazi kwa kuwasahilishia Watanzania mambo yao ambayo yanawaletea vigezo vya kujihusisha kwenye uhamiaji kwa kujenga nchi yao na kiuchumi.

Mh. Membe aligusia juu ya mambo ya uraia wa nchi mbili (Dual Citizenship) alisema serikali inajua kwa makini jambo hili na karibuni itafikia ukingoni kuliweka sawa suala hili la uraia wa nchi mbili. Alisema, kwasababu Serikali hii ya awamu ya nne ina masikio, na imewasikia Diaspora ya Watanzania wanaoishi ughaibuni.

Mh. Membe na Balozi mwanaidi Sinare Maajar na Naibu Balozi Chabaka Kilumanga na Twalane Migiro (pili shoto) mkutanoni.

Mh. Membe alimkurubia kila Mtanzania aliyehudhuria ili wapate ujumbe aliokuja nao. Pichani akionekana anaongea jambo akiwa pamoja na baadhi ya waliohudhuria mkutanoni.

Balozi Mwanaidi akiwa na Charles Hilary wa BBC (kulia) na Bwana Abbas wa Uhamiaji aliyekuja kutoa mada ya Diaspora 2.

Bi Mariam Senga (katikati) wa Ubalozi wa Tanzania nchini UK akiwa na mchezaji nyota wa zamani wa Yanga enzi hizo, Bwana Yanga Fadhili Bwanga (shoto) aliyetoka Abu Dhabi mahsusi kuhudhuria mkutano huu wa Diaspora 2.

Mwenyekiti wa TZUK anayemaliza muda wake Aboubakar Faraji (kulia) akiwa katika matayarisho ya kuwakilisha hotuba yake ya mwaka mbele ya Watanzania wanaoishi UK. Katikati ni Mwenyekiti wa muda aliyeshika usukani wa timu ya 'Task Force' kwa kuleta baadhi ya mabadiliko ya katiba Bi Norah Sumari na wengineo wa kutoka Ubalozini, n.k.

Caroline Chipeta akiweka mambo sawa kwa mume wake Wakili, Mh. Walter Chipeta ambaye aliwakilisha kuzungumza kwa kulichambua suala la uraia wa nchi mbili.

Mheshimiwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mwanaidi Maajar (kushoto) akifuatilia kwa makini mkutano wa Tanzania Diaspora 2 akiwa na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe na viongozi wengine.

Baadhi ya Diaspora ya Watanzania nchini UK waliofika mkutanoni ni Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association bwana Saleh Jaber (mbele watatu kulia) na bwana Farid Nassor (mbele wanne kulia) na bwana Ali (mbele wapili kulia) ambaye alijiwakilisha kama ni Mtanzania.

Wahudhuriaji mbalimbali walifika katika mkutano wa Diaspora 2.

Wajumbe waliofika kutoka Tanzania kuwakilisha makampuni na mashirika mbalimbali ya binafsi na serikali, wakisikiliza kwa makini katika mkutano wa Diaspora 2.

Wahudhuriaji mbalimbali walifika katika mkutano wa Diaspora 2 akiwamo Bi Sakina Dattoo (mbele wakwanza).

Mheshimiwa Issa Michuzi akimwaga nondo kwenye mkutano wa Tanzania Diaspora 2 nchini Uingereza akielezea vipi 'Social Media' inaleta mabadiliko ya kimaendeleo katika jamii.

Issa Michuzi akiwa na wajumbe mbalimbali wa Tanzania wanaoishi UK katika picha ya pamoja iliyochukuliwa siku ya kwanza ya mkutano wa Tanzania Diaspora 2, London. Pichani kushoto ni Sakina Dattoo na mbele wapili ni Bwana Haruna Mbeyu.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©