Mkataba wa kutandaza nyaya
za umeme Zanzibar
08/05/2010

Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.
Amani
Abeid Karume, Balozi wa Marekani nchini,
Alphonso E. Lenhardt, na viongozi wengine walikutana
katika kushuhudia utiaji saini mkataba wa kazi za ulazaji waya wa umeme
(Marine Cable) kutoka Ras Kiromoni, Dar es Salaam hadi Fumba.
Mtendaji Mkuu wa Millenium Challenge Tanzania,
Bernad Mchomvu alikuwa ni muwakilishi wa utiaji wa saini
na kukabidhiana mkataba na mwakilishi wa Kampuni ya Viscus ya nchini
Japan, bwana
Tesuji Onno. Kazi hiyo
inatarajiwa kuanza hivi karibuni kwa kuimarisha huduma za umeme
Zanzibar.
|