Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Meya wa Mwanza ahojiwa juu ya mauaji ya Bi Bahati

20/05/2010

Kufuatia mauaji ya utata ya Bi Bahati Stephano yaliyotukia jijini Mwanza, Kamanda wa polisi jijini humo bwana Simon Siro amesema, "...Jana jioni majira ya saa kumi pale Uwanja wa Ndege wa Mwanza tuliweza kumkamata mheshimiwa Leonard Bandiho Bihondo (pichani juu) ambaye ni mstahiki Meya wa jiji la Mwanza ana umri wa miaka 64 kwa tuhuma hii ya mauaji ya Bi Bahati Stephano aliyekuwa katibu wa CCM Isamilo jijini Mwanza.

Hii imekuja mara baada ya kufanya mahojiano na watuhumiwa wote watatu ambao tayari tumekwisha wakamata, wote wamekuwa wakimtaja kwamba ndiye anayehusika katika tukio hili. Kwa hiyo, mahojiano yanafanyika ili tuweze kujua ukweli wa tuhuma hizi na kama tutathibitisha bila mashaka kwamba anahusika na mauaji haya aidha kwa kula njama au kwa, au kwa njia nyingine basi tutampeleka mahakamani na sheria kuchukua mkondo wake. Lakini niombe kwamba bado tunahitaji taarifa nyingine nyingi maana tunajua suala la kesi ya mauaji ni kubwa na linahitaji ushahidi ulio mkamilifu toka pande zote mbili kwa lengo la kuhakikisha kwamba hatutomwonea mtu yeyote ili kulinda haki ya kila mtu na kuhakikisha kwamba hakuna mtu aliyeko juu ya sheria."

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©