Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Safari ya Vifaru sita kurudi Afrika yaanza

24/05/2010

Hatimaye ile safari ya kurejesha vifaru weusi 6 na wengine hadi watakapotimia 32 kutoka nchini Afrika Kusini hadi Tanzania imeanza na inatarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitatu.

Hii si mara ya kwanza kwa vifaru kurejeshwa Tanzania toka ugenini kwani mwaka jana vifaru wengine walirejeshwa toka nchini Czech.

Vifaru hao wanarejeshwa katika mbuga ya Wanyama ya Taifa iliyoko Serengeti baada ya wazazi wao kuchukuliwa mwaka 1961 kutoka Tanzania ili kuwalinda dhidi ya kutoweka kutokana na uwindaji wa kinyume na sheria. Vifaru weusi ni mojawapo ya viumbe waliojumuishwa katika kundi la wanyama waliomo katika hatari ya kutoweka katika uso wa dunia. Inaripotiwa kuwa nchini Tanzania, idadi ya vifaru wa aina hiyo ni 70 tu. Ikiwa utaratibu huo utafanikiwa kama ilivyopangwa, basi eneo la hifadhi ya wanyama pori la Serengeti-Mara ndilo litakalokuwa na hifadhi kubwa kuliko zote duniani la vifaru weusi.

Gharama za kuwarejesha vifaru kutoka Afrika Kusini hadi Uwanja wa Ndege wa Kilimanjaro (KIA) kisha kusafirisha kwa barabara hadi hifadhi ya Ngorongoro hao zinakadiriwa kuwa dola za Kimarekani laki moja ($100,000). Hifadhi ya Taifa ya Wanyamapori ya Ngorongoro tayari ina vifaru wapatao 24 ambao wana vifaa maalumu vya ulinzi (GPS) ambavyo hurekodi nyendo zao na mahali walipo kila wakati ili hivyo kuwalinda dhidi ya hatari na wawindaji wa wanyama kinyume na sheria wanaosaka pembe zao ambazo huuzwa katika masoko ya kinyume na sheria barani Asia. Uwindaji wa kinyume na sheria umeangamiza asilimia 90% ya vifaru weusi katika kipindi cha miaka 40 (mwaka 1970 ilikadiriwa kuwepo vifaru weusi 60,000 barani Afrika). Kutokana na ulinzi madhubuti, idadi ya vifaru hao imeendelea kuongezekana sasainakadiriwa kuwa wapo vifaru weusi wapatao 4,200 barani Afrika na inatarajiwa kuwa vifaru hao watakapofika Tanzania, basi idadi yao itaendelea kuongezeka.

Usimamizi wa utaratibu mzima wa kurudishwaji viboko hao utasimamiwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Utalii na Maliasili ya nchini Afrika Kusini --South African National Parks (SANParks), Shirika la Hifadhi ya Wanyama Pori Tanzania, Tanzania National Parks (TANAPA), na Shirika la Utafiti wa Viumbemwitu Tanzania, Tanzania Wildlife Research Institute (TAWIRI), na shirika la Frankfurt Zoological Society (FZS) la nchini Ujerumani.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©