Brazil 5 Tanzania 1
08/06/2010

Heka heka langoni

Mpira umetinga wavuni

Kipa anajizoa chini

Shangwe na manyago golini. Picha na
Issa Michuzi
Habari Kamili
Aliyeongoza kufungua kitabu cha magoli ni
Robinho aliyeifungia timu yake bao kunako dakika ya 10. Ilimchukua tena
Robinho takriban dakika ishirini hivi ambapo dakiak ya 33 aliiandikia
timu yake bao la pili ambalo lilidumu hadi kipindi cha kwanza kumalizika.
Kipindi cha pili kilianza na mnamo dakika
ya 52 mchezaji wa Brazili Ramires, aliifungia timu yake bao la tatu.
Mchezaji machachari wa Brazili, Kaka, ambaye kwa takriban mwaka mmoja
alikuwa hajaifungia bao lolote timu yake ya taifa alifanikiwa kufuta
nuksi hiyo pale alipachika bao katika dakika ya 75 ya mchezo.
Ilikuwa ni mchezaji Aziz aliyeusindikiza
vyema mpira uliochongwa kutoka kwenye kona na hivyo kuipa Tanzania
kifutia machozi kunako dakika ya 85 ya mchezo.
Ndani ya dakika tatu za majeruhi, zikiwa
zimesalia dakika mbili na ushee, ilikuwa ni Ramires aliyeamua kuonesha
kuwa 'alikuwepo' kwa kupachika bao lake la pili na la 5 kwa timu yake ya
Brazil.
Hivyo hadi kipenga cha mwisho kinali, ni
Brazil 5 Tanzania 1.
Mrisho Ngassa aling'ara katika muda wote
aliocheza lakini jitihada zake ziliishia mikononi mwa kipa wa Brazili au
kutolewa nje. Mchezaji Jerson "Jerry" Tegete aliingia dakika chache
kabla ya mechi kwisha na kuchukua nafasi ya Ngassa lakini naye
hakufanikiwa kupata goli.
Timu ya Brazili ilishusha nyota wake ambao
wanaunda kikosi kitakachoshiriki katika michuano ya kuwania kombe la
Dunia kwa mchezo wa soka.
|