Kocha mpya wa Taifa Stars
JAN BORGE POULSEN
10/06/2010

Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa
miguu nchini Tanzania (TFF) Fredrick Mwakalebela emamtangaza kocha mpya
wa timu ya taifa ya Tanzania kuwa ni bwana Jan Borge Poulsen.
Kocha huyo ambaye ni raia wa Denmark ana
wasifu wa kuichezea timu ya taifa ya Denmark na kufundisha timu
mbalimbali za taifa katika bara la Asia na Ulaya.

Jan Borge Poulsen (pichani) amepewa
mkataba wa miaka miwili kuifundisha Taifa Stars kuanzia mwezi Agosti,
2010.
|