Aliyemkubatia KAKA katika
mechi ya Tanzania na Brazil
12/06/2010

Kijana Nagery Ally Kondo (pichani juu)
alifika katika studio za redio Clouds FM na kuhojiwa katika kipindi cha
Power Breakfast Juni 10, 2010 na Dina Marios anaandika hivi katika blogu
yake "...wakati wanaenda uwanja wa taifa yeye na wenzake walikata tiketi
ya Tsh 30,000 lakini kutokana na kutokuwa na watu Maaskari waliwaruhusu
kukaa jukwaa la Tsh 80,000....mpira ulipokolea Washikaji zake walimuona
jamaa anavua mkanda, saa, viatu akawaomba wamshikie simu na kuwaambia
mie naenda hivyo kumkumbatia Kaka. Wenzie walijua utani mara jamaa
akaanza kukimbia akielekea uanjani na kwenda kumkumbatia Kaka.Na anasema
wakati anaenda alikuwa anajua lazima yatampata makubwa lakini alishaamua
potelea mbali Mzuka wa soka ushampanda liwalo na liwe.
Anasema hakupanga chochote toka anatoka
nyumbani mzuka ulimpanda wakati anaangalia soka hapo uwanjani na
akajikuta anatamani kwenda kumkumbatia Kaka na ndicho alichofanya." - Dina
Marios.
Watu kadhaa wametoa hisia mchanganyiko kuhusiana
na tukio hili. Baadhi wamesema kuwa kwa kuwa alikuwa na nia njema na kwa
kuwa kitendo kama hiki hutokea kwingineko duniani, basi adhabu yake
isiwe ya kutisha. Wapo waliohoji umakini wa askari katiak kazi yao
kuhusiana na hili. Vile vile wapo waliasa kuwa endapo kijana huyu angekuwa
ameficha silaha na kumdhuru yeyote kiwanjani, ingechafua kabisa nchi ya
Tanzania na hili laweza kutokea kwani mtu anaweza kuficha silaha popote
na kuitumia haraka.

Nagery Ally Kondo akijitosa uwanjani...

Kwa raha zake...

Lengo lake ni kumkumbatia KAKA tu...

Hatimaye azma yake imetimia, KAKA bia
ajizi amkumbatia Ally Kondo...

Sasa lengo limetimia ni wakati wa kuondoka
mechi iendelee...

mkono kwa mkono, bega kwa bega...

Haya sasa nenda bwana Kondo tuendelee na
boli...

Oyeee! nimetimiza azma yangu...

Kwa heri bwana Kondo...

Shadarack Nsajigwa (namba 14) kapteni wa
Taifa Stars akishangaa jamaa aliyejitosa kwenda katikati ya uwanja
kumkumbatia KAKA wakati mechi inaendelea...

Ya mwisho mwishooo...

Kwaherini...

Sasa nipelekeni kokote sina neno, azma
yangu nishaitimiza...

Sijapata kufurahi maishani mwangu kama leo...

Twende zetu huku tukazungumze kwa kituo...

Kijana wetu huyu hana tatizo huyu, ni
mshabiki tu kama mashabiki wengine, lakini tunaye...

Nagery Ally Kondo (21) akiwa ndani ya
ofisi za Clouds FM Radio katika kipindi cha 'Power Breakfast' na Gerald
Hando (shati jekundu) na Paul James (PJ) mwenye kofia.
|