Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Matayarisho ya Sabasaba 2010

13/06/2010

Hili ndilo Bango la matangazo linaloonekana katika geti kuu la kuingilia katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, kwenye maonyesho ya Sabasaba 2010.

Mafundi wakiwa katika shughuli za ujenzi na ukarabati wa sehemu za viwanja hivyo ili kuweka sawa kabla ya kuanza maonyesho hayo yanayotarajia kuanza Julai mosi mwaka huu.

Hawa pia ni mafundi wakikokota mbao zao kwa ajili ya kwenda kujengea vibanda ndani ya viwanja hivyo.

Wafanyakazi wa kukodishwa katika ujenzi na ukarabati wa mabanda ya Maonyesho ya Saba Saba wakiendelea na ujenzi ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya Maonyesho hayo yanayotarajia kuanzanza Julai 1 mwaka huu.

Katika kazi hakuna kuremba, hata kina mama wameweza kujitokeza kwa wingi katika viwanja hivyo na kushirikiana na mafundi wa kiume katika ujenzi na ukarabati na wengi wao wamekuwa wakibeba zege na mchana viwanjani humo ni ilimradi tu mkono uende kinywani siku hizi wanawake pia hawachagui kazi hivyo ukiwa na kazi yoyote usisite kumshirikisha mwanamama kwa kuhofia anaweza kukataa, ila iwe kazi halali.

Haya ni mabanda yaliyotumiwa na Wizara ya Afya katika maonyesho ya mwaka jana, ambayo pia yako katika hali nzuri baada ya kufanyiwa ukarabati wa hali ya juu na wa kupendeza kama yanavyoonekana.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©