Rais Kikwete apokelewa kwa
shangwe Kigoma
17/06/2010

Baadhi ya wakazi wa
kigoma wakimlaki Rais Kikwete kwa ngoma za utamaduni baada ya kuwasili
katika uwanja wa ndege wa Kigoma kwa ziara ya kikazi ya siku mbili
mkoani humo.

Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akisalimiana na mtoto ambaye jina lake halikuweza kupatikana
mara moja muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kigoma
kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akikata utepe kufungua rasmi hoteli ya Lake Tanganyika mjini
Kigoma. Kushoto ni Mmiliki wa hoteli hiyo Bwana George Nzunda na kulia
ni Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Simbakalia.

Rais Jakaya Mrisho
Kikwete akikagua mandhari ya Hoteli ya Lake Tanganyika muda mfupi baada
ya kuifungua mjini Kigoma. Kulia ni Mmiliki wa Hoteli hiyo Bwana George
Nzunda na katikati ni Mkuu wa Mkoa wa kigoma Kanali Simbakalia.
|