Tahadhari na uegeshaji
gari
20/06/2010

Kila ifikapo jioni, 'Askari' huyu hupita
mtaa wa Samora kuelekea Makao Makuu ya Polisi Wizara ya Mambo ya Ndani
ya Nchi kuchukua wafanyakazi.

Hivyo, njiani akilikuta gari limeegeshwa
njiani hata kwa dharura, hulitoa upepo.

Akiwa kamaliza kazi yake, sasa anaendelea
na safari yake.

Wengi wamekubwa na adha hiyo ingawa siku
moja inadaiwa alimtolea upepo bosi wake bila ya yeye mwenyewe kujua...
Hivyo watumiaji wa barabara hiyo kuweni makini na kadhia hii ya kutolewa
upepo magari.

Na hii ni Zanzibar, katika majumba ya
Michenzani. Ikionekana pichani kigari cha kubebea mizigo ikiondoa gari
katika maeneo ya Michenzani kupisha matengenezo makubwa ya barabara ya
Michenzani-Mlandege.

Gari lingine likipigwa kijiko mbele ya
jumba namba Tano la Michenzani, Zanzibar.
|