Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Clinton azuru Tanzania

23/06/2010

Raisi Jakaya Kikwete amefanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Marekani, Bill Clinton ambaye amekuja Tanzania kutembelea na kuangalia shughuli zinavyoendelea katika mfuko wake unajishughulisha na shughuli za upatikanaji wa huduma za afya duniani, Clinton Health Access Initiative (CHAI).

Katika mazungumzo yao, pamoja na Rais Kikwete kumshukuru Clinton kwa mchango wake hapa nchini kwa sekta ya afya, viongozi  hao walizungumzia hali ya kisiasa na maendeleo ya Tanzania.



Mchango huo wa Clinton hapa nchini ni katika masuala ya HIV/AIDS ambapo mfuko wa Bill Clinton unasaidia kutoa dawa za kupunguza makali na athari za Ukimwi (ARVs).

Clinton amekuwa mstari wa mbele katika kuchangia kampuni nyingi kupewa nafasi ya kutengeneza dawa za ARV na hivyo kuweza kushuka kwa bei na hatimaye watu wengi hasa katika nchi masikini kuweza kumudu bei ya dawa hizo.



Kutokana na jitihada hizo serikali imeweza kuanzisha mpango wa kitaifa wa huduma na matibabu wa mwaka 2003 (National HIV/AIDS Care and Treatment Plan 2003), mpango ambao umeandaliwa kwa pamoja baina ya serikali na CHAI.

Mpango huu unalenga kuhakikisha kuwa watu waishio na virusi vya Ukimwi wanapata huduma na dawa bila kujali hali zao za kiuchumi au uwezo.

Mfano wa Juhudi za CHAI za kuhakikisha huduma za afya zinapatikana ni  katika Mikoa ya Lindi na Mtwara ambapo waathirika wanapata huduma za awali ikiwemo vipimo na dawa  katika vituo vya maabara ya kisasa huko huko vijijini, wilayani na Mikoani. Pamoja na dawa, CHAI pia inatoa mafunzo kwa maafisa wa afya wanaotoa huduma.

Jana mchana Clinton alitembelea kituo cha Afya cha Kitere kilichoko Mtwara Vijijini na kurejea jijini jioni. Clinton ataondoka nchini leo kuelekea Afrika Kusini.

Bill Clinton alizindua rasmi mradi wa CHAI tangu mwaka 2007 bonyeza hapa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©