Madawa ya kulevya yaliyokamatwa ni aina
ya Cocaine yanayokadiriwa kuwa na uzito wa kilogramu 31. Madawa hayo
yalikamatwa wakati watuhumiwa walipofika katika Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tarehe 23 Juni 2010
wakitokea nchini Afrika ya Kusini na ndege namba SA 199.
Watuhumiwa hao walikuwa wamebeba
mabegi yenye nembo za kidiplomasia (Diplomatic Bag) ili kupunguza
uwezekano wa kutokukaguliwa lakini askari waliwashuku na walipohojiwa walidai
kuwa wao ni wanadiplomasia wanatoka Ubalozini, pamoja na majibu hayo,
askari waliwatia mashaka na hivyo kuamua kuwapekua na kuwakuta na
madawa hayo. Watuhumiwa wapo mahabusu kwa upelelezi zaidi.

credit: Muhidin Sufiani/sufiani
mafoto blog na Baraka Mfunguo/mtwara
kumekucha blog
YATOKANAYO
Madhara ya matumizi holela ya madawa ya kulevya ni makubwa na
yamezidhuru jamii zote duniani. Familia nyingi zimeparaganyika
kutokana na madhara haya. Ni jukumu la wananchi kupambana ili kuzuia
madhara ambayo yanaathiri hata wale wasiohusika moja kwa moja kwa
mfano, wizi na udokozi wa vitu na kuviuza ili kupata fedha ya
kununulia madawa ya kulevya ili kukidhi haja ya mwili. Wapo wazazi,
wazee na watoto ambao wameumizwa na vijana wanaotumia madawa ya
kulevya. Pia, zipo familia zilizogombana, zilizotengana na hata watu
kufa kwa sababu ya athari ya biashara au matumizi ya madawa ya
kulevya.