Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ajali ya Ngalawa Dar es Salaam

28/06/2010

litokea ajali ya boti ya Seagull kuigonga ngalawa iliyokuwa ikipita karibu yake. Waliokuwa kwenye ngalawa waliokolewa japo chombo chenyewe kilizama majini. Haijaripotiwa kupotea uhai kwa yeyote katika ajali hiyo.

Watu 11 wamenusurika kufa maji, baada ya ngalawa yenye jila la Usilolijua, kugongana na boti ya Kampuni ya Sea Gull, ya Zanzibar. Ajali hiyo iliyohusisha jahazi linalofanya biashara ya kusafirisha vinywaji aina ya bia na bidhaa nyingine kutoka Dar es Salaam kwenda Zanzibar, ilitokea saa 7:00 mchana. Hata hivyo wakati ajali hiyo inatokea, jahazi lilikuwa na  kreti tupu 1,400 za bia na ilikuwa inakuja Dar es Salaam kubeba bia.



Nahodha mkuu wa jahazi, Musa Machano (35), alisema wamepoteza kreti zote, nguo, viatu, simu na fedha taslimu Sh180,000 baada ya jahazi kugongwa wakati wanakaribia kufika eneo la kutia nanga. Machano alisema kabla ya tukio hilo, alishaonyesha ishara ya bendera kwa nahodha wa boti ya Sea Gull kuashiria kuwa alikuwa katika eneo hilo na kwa hiyo apunguze mwendo na kubadili njia, lakini haikusaidia.



"Nilimuonyesha nahodha mwenzangu ishara kwamba niko eneo lile, lakini haikusaidia kwa sababu aliendelea kuja kwa mwendo ule ule aliokuwa nao na kunigonga sehemu ya ubavuni upande wa kulia,"alisema Machano. "Tunawashukuru wenzetu kwa msaaada waliotupa kwani bila wao kile kitambaa kilichokuwa kimetufunika kingeweza kutusababishaia vifo," alisema. "Hii jahazi yetu inategemea upepo si kama boti ya mwenzetu inayotumia mashine. Nilipomuonyesha ishara mwenzangu alitakiwa kunikwepa na kupita sehemu nyingine lakini badala yake alitugonga kwa makusudi,"alisema Machano.

Alisema ndani ya jahazi kulikuwa watu 11. Aliwataja wenzake waliokuwemo kwenye jahazi hilo kuwa ni, Kaimu Amri (50)Musa Machano(35)Hamis Abdalah(18)Hamis Makame(14) Nasoro Muhamed(15). Wengine ni Rashd Fumo(15), Hamis Shauri(24),Haji Sahaban (22) na mmoja aliyetambulika kwa jina moja la Mati (32).

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alifika katika eneo la tukio na kuzungumza na watu walionusurika na kuahidi kuwanunulia simu kwa kila mmoja, baada ya simu zao kuzama majini. "Wakati tunaendelea kuwasiliana na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) kuangalia sheria za ajali ya majini zinasemaje  kila mmoja nitampa simu nyingine,"alisema Kova.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©