Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mama Salma azindua ukarabati sekondari Tabora

29/06/2010

Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amezindua rasmi awamu ya kwanza ya ukarabati na upanuzi (Rehabilitation and Extension) wa shule ya sekondari ya wasichana ya Tabora unaofanywa kwa hisani ya Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) kwa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 1.7. Waliohudhuria uzinduzi huo ni wanafunzi wa shule za Tabora Wasichana, Tabora Wavulana na Mirambo pamoja na walimu na Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Abeid Mwinyimsa.

Mke wa Rais, Mama Salma Kikwete, akiwahutubia wanafunzi wa shule za Sekondari za Mkoa wa Tabora wavulana na wasichana na Mirambo wakati wa sherehe za uzinduzi wa upanuzi na ukarabati wa shule ya sekondari Tabora wasichana uliofanyika jana mkoani humo.

Mama Salma Kikwete akitembelea moja ya bweni lililokarabatiwa katika shule ya wasichana ya Tabora baada ya kuzindua mradi wa ukarabati na upanuzi wa shule hiyo.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©