Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ndege yaanguka Tanga

30/06/2010

Kwa mujibu wa taarifa ya habari ya mchana kupitia TBC1, ndege ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) ya kituo cha Ngerengere mkoani Morogoro imeanguka katika eneo la Manga-Kabuku mkoani Tanga.

Ndege hiyo ilikuwa katika mazoezi na ilipata hitilafu hivyo ikabidi kutua kwa dharura katika barabara na hivyo kusabisha kugongana uso kwa uso na basi lililokuwa limebeba watalii lililokuwa katika eneo hilo la barabara.



Ndege hiyo ilikuwa imebeba watu watatu ambapo wawili walikuwa ni marubani na mmoja wao alifariki papo hapo. Imeripotiwa kuwa hakuna abiria yeyote katika basi la utalii aliyepoteza uhai.

Ndege hiyo imesababisha barabara isipitike na hivyo kukwamisha usafiri kwa abiria wanaotoka na kuingia kwa kutumia barabara inayounganishwa na mikoa ya Kaskazini na ile inayounganishwa na mkoa wa Pwani.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©