Ndege hiyo
iliruka katika Uwanja wa Ndege wa
Zanzibar, Kiembesamaki nje kidogo ya mji
wa Zanzibar, siky ya Ijumaa, Oktoba Mosi
majira ya saa 3.44 asubuhi, na ilipofika
eneo hilo saa 3.55, ilipata hitilafu
ikiwa angani, ndipo rubani akaamua
kutua barabarani. Rubani huyo na
mwanafunzi wake walisalimika ingawa
ndege ilipata athari kidogo kutokana na
kuingia kwenye msingi wenye mawe.
Sumry
alisema ndege hiyo yenye namba 5H-TFS
aina ya Piper 28-140, kwa kawaida
hutumika kuwapa mazoezi marubani
wanafunzi katika eneo hilo, kutokana na
kutotumiwa na ndege nyingine.
Hili ni
tukio la pili kwa mwaka huu kwa ndege
kutua barabarani kwa dharura. Mapema
mwaka huu, ndege ndogo kama hiyo ilitua
katika barabara ya Kiwengwa mkoa wa
Kaskazini Unguja. Miaka kadhaa
iliyopita, ndege ndogo ya kampuni hiyo
ya Tropical Air iliwahi kuanguka
baharini karibu na kisiwa cha Chumbe,
wilaya ya Kusini Unguja, ikiwa na abiria
wawili, mtu na mkewe.