Lakini pia Dhumuni letu
ni kuuunga mkono
jitihada za serikali
chini ya Wizara ya Elimu
katika kuendelea kukuza
kiwango cha elimu nchini
kwa kuziwezesha ngazi
mbalimbali tukianzia na
shule za msingi kwa
kupambana na changamoto
zinazokabili sekta hii.
Leo hii Tigo tunajisikia
fahari sana kutoa
mchango wetu huu
kusaidia wanafunzi ambao
tunaamini ndio taifa la
kesho.
Mheshimiwa Naibu Katibu
mkuu Wizara ya elimu na
Mafunzo ya Ufunzo ya
Ufundi, Tigo tunachukua
nafasi hii kukufahamisha
rasmi kuwa makabidhiano
ya Basi hili ni
muendelezo wa mikakati
madhubuti tuliyopanga
tangu awali ya
kuhakikisha tunasaidia
jamii tunayoihudumia
kwenye biashara yetu.
Tigo tunatambua sana
umuhimu wa wateja wetu
hivyo tumejikita
kusaidia jamii kwenye
swala la Elimu, Afya,
Mazingira, Kampuni ya
Simu za mkononi Tigo
imekua ikisaidia jamii
kwenye sekta ya
mawasiliano kwa kutoa
huduma bora kwa
kuzingatia zaidi unafuu
wa huduma kuliko mtandao
wowote nchini.
Pia katika elimu ya
jamii na afya mwezi
uliopita tu Tigo
imechangia zaidi ya
shilingi milioni 76 kwa
hospitali ya CCBRT
kuchangia mradi wa
kupima na kutibu macho
bure utakaoanza
kufanyika kule Mwanza
mwezi huu na pia
kufundisha wakunga jinsi
ya kuhudumia jamii kwa
hospitali mbalimbali.
Kwaniaba ya Tigo
ninaomba nitangulize
shukrani zangu kwa wewe
kukubali kutenga muda
kwaajili ya kuungana
nasi katika tukio hili
la kijamii na la
kihistoria ili kuboresha
elimu nchini.