Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Mechi ya kimataifa bila ya wimbo wa Taifa

11/10/2010

Shirikisho la soka Tanzania, TFF, limemsimamisha kazi msemaji wake Florian Kaijage (pichani) baada kushindwa kupiga nyimbo za taifa katika mchezo wa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika kati ya Morocco na Tanzania.

Kabla ya kuanza kwa mechi ambapo Rais kikwete alikuwa mgeni rasmi, baada ya kukagua timu na kusubiri nyimbo za taifa, hakuna kilichosikika.

Mpaka sasa bado haijafahamika kwanini nyimbo hizo zilishindwa kupigwa. Kufuatia kitendo hicho, TFF imeamua kumsimamisha kazi msemaji wa TFF, Florian Kaijage kwa kuwa ndiye aliyekuwa amepewa jukumu la kusimamia jambo hilo, mpaka hapo uchunguzi utakapokamilika.

Rais wa TFF, Leodegar Tenga amesema kwa kushirikiana na Wizara ya Habari Utamaduni na michezo, wanaunda kamati itakayochunguza chanzo cha tatizo hilo huku Kaijage akiwa nje mpaka uchunguzi utakapokamalika. Akaongeza kusema kuwa tukio hilo ni la aibu mbele ya Rais Jakaya Kikwete, washabiki na wageni wengine na mbaya zaidi kwa vile mchezo huo ulionyeshwa katika luninga ndani na nje ya nchi, hivyo aibu hiyo imeshuhudiwa na wapenzi wa soka kote duniani.

“Kushindwa upigaji nyimbo za taifa ni upungufu mkubwa kiutendaji na kama nilivyosema hapo awali ni aibu kwa taifa letu, napenda kwa niaba ya TFF kuomba radhi kwa Mheshimiwa Rais, wapenzi waliofurika uwanjani, Watanzania kwa jumla na wageni wetu kutoka Morocco” alisema Tenga.

Amesema jambo hilo halikustahili kutokea kwa kuwa liliishawahi kutokea wakati wa mechi na Brazil ambapo wahusika walionywa na kupewa jukumu la kuhakikisha wanazijaribu nyimbo zote siku mbili kabla ya mchezo na kuhakikisha kuwa hakuna hitilafu yoyote na wahusika walimuhakikishia kuwa hakutatokea dosari yoyote.

Alisema kuanzia sasa, hata kama mitambo ya uwanjani ni mizima, patakuwepo bendi za Polisi/Jeshi ama mitambo ya tahadhari kwa ajili ya nyimbo za taifa na matangazo mengine muhimu.

Aidha, katika hatua nyingine Tenga amesema ndani ya mwezi mmoja TFF inatarajia kutangaza nafasi mbili za ajira zilizoachwa wazi, ambazo ni ya sasa ya Msemaji wa shirikisho hilo na ile ya Katibu wa TFF ambapo awali ilikuwa ajira ya Frederick Mwakalabela ambaye alijiengua ili kugombea Ubunge wa Iringa Mjini (CCM).

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©