Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ada kuanza kutozwa kuegesha gari nje ya jiji

15/10/2010

Kampuni ya Maegesho ya Taifa (NPS), inatarajia kuanza kutoa huduma ya uegeshaji kwa kutumia mfumo wa mashine maalumu utakaosaidia kuongeza mapato na pia kupanua huduma zake katika maeneo mengine ya Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza juzi, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni hiyo, Hassan Khan, alisema utaratibu wa kutumia mashine hizo unatarajia kuanza rasmi Novemba 15.

Alisema, mashine hizo ambazo zitatumika kwa mara ya kwanza nchini na Afrika, zitaongeza kipato kwa kuwa zitadhibiti mapato yatokanayo na uegeshaji.

Khan alisema, mashine hizo zitakuwa za aina mbili, moja ikiwa ni ndogo itakayokuwa ikishikwa na wahudumu mikononi huku nyingine zikifungwa mitaani kwa ajili ya waegeshaji kujihudumia wenyewe.

“Kwa kuanza, hizi mashine za mitaani zitahudumiwa na watoa huduma wetu, kwamba mwegeshaji atamkabidhi ada ya uegeshaji na kuitumbukiza kwenye mashine na kumpa tiketi yake,” alisema Khan.

Alisema lengo la kufanya hivyo ni kuondoa udanganyifu unaoweza kufanywa na mwegeshaji.

“Unajua hata Ulaya, watu wa aina hiyo wapo, mtu badala ya kuweka fedha halali anatumbukiza hata fedha za aina tofauti na zilizokusudiwa,” aliongeza Khan.

Kuhusu kupanuka kwa huduma za uegeshaji, alisema baada ya kuanza kazi kwa huduma hizo, watakwenda hadi pembeni mwa Jiji na kutoza ushuru wa uegeshaji.

“Maeneo yote ambapo pia kuna utaratibu wa kuegesha magari bila mpango tutaanza kukusanya ushuru wa maegesho; Tegeta, Mbezi na maeneo mengine mengi yaliyopo pembeni mwa mji, kabla ya hapo mapato yalikuwa yanakusanywa Kariakoo na katikati ya Jiji,” aliongeza Khan.

Aidha, alisema wanatarajia kuongeza idadi ya wafanyakazi hadi 1,000 kwa ajili ya ufanisi wa kazi hiyo, ambapo kwa sasa alisema kampuni hiyo ina wafanyakazi 355
.

Mfumo huu pengine ni mzuri kwa kudhibiti magari na kwa mapato, lakini la kujiuliza ni kuwa si wananchi wote wenye uwezo wa kulipishwa ada hizo ambao wao wenyewe mapato yao ni madogo kwa maisha yao hasa pembeni mwa mjini na nje kidogo ya jiji. Na si suala la kufananishwa na Ulaya, angalau kwa sasa.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©