“Tunawataka wananchi wenye matatizo
mbalimbali kujitokeza katika meli hiyo
na kupatiwa matibabu kwa matatizo
mbalimbali yanayowasumbua,“ alisema
Xinsheng.
Alisema
meli hiyo itatoa huduma za vipimo,
ushauri, tiba ya asili kutoka China
pamoja na tiba ya kisasa na upasuaji
mkubwa na mdogo.
Alisema
meli hiyo inayoitwa ‘Ark Peace’ ina
vitanda 500 na vyumba vya upasuaji
vinane kwa ajili ya kutoa huduma ya
kulaza wagonjwa watakaoonekana kuwa
wanahitajika kupewa huduma hiyo na
kwamba huduma zote zitafanyika ndani ya
meli.