Mchezaji
wa timu ya soka ya Yanga, Jerry Tegete
amemchoma Simba mkuki mmoja na kumwacha
na bandeji yake kunano dakika ya 71
katika mchezo wao uliochezwa kwenye
kiwanja cha Kirumba jijini Mwanza.
Simba
ndiyo wa kujibebesha lawama wenyewe
kwani waliotizama mechi wanasema timu
ilikosa nafasi nyingi sana za wazi
lakini nafasi ya mtende waliyoipata
Yanga hawakuifanyia ajizi na ndiyo
iliyozaa goli la mechi.
Katika
mechi hiyo, Kocha wa Yanga, Papic
alitolewa nje ya uwanja na mwamuzi. (samahani
sikutizama mechi hivyo sina taarifa
kamili ya iliyokuwa sababu hasa ya
kutolewa nje kwa kocha huyo).
Timu zote
(Simba na Yanga) sasa zinakuwa
zimeshacheza michezo 8 ambapo Yanga
inaongoza ligi kwa kuwa na pinti 19
ikifuatiwa na Simba yenye pointi 15 na
nafasi ya tatu ipo kwa JKT Ruvu kwa
pointi 11 za mechi 6.