Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Ofisi na makazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania iliyopo Zanzibar

18/10/2010

Hili ndilo jengo la Ofisi ya Makamu wa Rais wa Tanzania lilofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume, lilioko katika eneo la Tunguu nje kidogo ya Mji wa Zanzibar.

MAFANIKIO makubwa yataendelea kupatikana katika taasisi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendelea kujenga majengo ya afisi zake hapa Zanzibar ili kuimarisha na kufanikisha utendaji wa kazi za taasisi hizo.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Amani Abeid Karume aliyasema hayo mara baada ya kulifungua jengo la afisi na makazi ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huko Tunguu nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Rais Karume alisema kuwa umuhimu wa kujenga afisi hizo unakuja kutokana na kuongezeka haja na shughuli za afisi hizo, katika kuimarisha utekelezaji wa kazi na mambo ya Muungano.

Katika hotuba yake, Rais Karume aliipongeza afisi ya Makamu wa Rais chini ya uongozi wa Dk. Ali Mohammed Shein, kwa kujenga jengo hilo la kisasa hapa Zanzibar, ambalo ni kielelezo cha mapenzi yao kwa Zanzibar.

Aidha, Dk. Karume alimpongeza na kumshukuru aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), marehemu Daud Balali kwa uwamuzi wake wa kujenga afisi ya kisasa ya taasisi hiyo hapa Zanzibar.

Mbali ya kusifia usanifu na ujenzi wa jengo hilo, Dk. Karume alihimiza utunzaji wa majengo hayo na kueleza umuhimu wa kutengwa bajeti maalum ya matunzo na uendelezaji wake.

Akizungumzia ujenzi wa afisi na makaazi hayo, Katibu Mkuu afisi ya Makamu wa Rais, Ruth Mollel, amesema kuwa ujwenzi huo umegharimu zaidi ya shilingi za Tanzania, bilioni 10.3, ambapo zaidi ya bilioni 8.6 ni kwa ujenzi na zaidi ya bilioni 1.7 ni za utaalamu.

Mollel alieleza kuwa ujenzi huo ulioanza Julai 2007 na kumalizika mwaka huu, umefanywa chini ya Ukandarasia wa Kampuni ya Railway Chianchang Engineering ya China na kusimamiwa na Chuo Kikuu cha Ardhi cha Dar-es-Salaam.

Aidha, Katibu Mkuu huyo alitoa shukurani kwa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Rais Karume kwa kupewa eneo hilo kwa ajili ya ujenzi huo wa afisi na nyumba ya makaazi ya Makamu wa Rais.

Nae Waziru wa Nchi Afisi ya Makamu wa Rais (Muungano), Mohammed Seif Khatib, alisema ujenzi wa afisi hiyo ni muendelezo wa hatua za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kujenga afisi zake za kudumu hapa Zanzibar.

Alizitaja miongoni mwa afisi hizo kuwa ni Afisi ya Uhamiaji Mkoa wa Kusini Unguja, jengo jipya linalojengwa la Afisi Kuu ya Uhamiaji Zanzibar, jengo jipya la afisi ya Bunge, nyumba ya kulala wageni huko Madungu Pemba na jengo la Benki Kuu lililopo Gulioni mjini Zanzibar.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©