Mwana
blogu Mubelwa Bandio alihudhuria
uzinduzi wa blogu ya
http://lukemusicfactory.blogspot.com
ambapo anasema, ilikuwa nii zaidi ya
uzinduzi...., Ni zaidi ya maonesho....
yaani, ni mjumuiko wa Watanzania na
utambulisho wa ujasiriamali wa
Watanzania, kwa Watanzania.
Mheshimiwa
Balozi akipokelewa na waandaaji wa
uzinduzi huo Usiku wa kuamkia leo,
uliofanyika katika ukumbi wa Mirage Hall
mjini Hyattsville, jimbo la Maryland
Marekani.
Blogu ya
Vijimambo ambayo ilianza Januari 31
mwaka huu, iliandaa uzinduzi wake rasmi
ambapo mgeni wa heshima alikuwa ni
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania nchini Marekani Mhe. Mwanaidi
Maajar na pia ilihusisha "maonesho" na
maelezo ya bidhaa toka kwa wadau
wahusikao na jamii ya Watanzania hapa
nchini (kama Idhaa ya Kiswahili ya Sauti
ya Amerika), mwanamitindo maarufu nchini
Tanzania mama Asia Idarous na
wajasiriamali wengi sana waTanzania
wafanyao shughuli zao hapa nchini.
Mara baada
ya kuwasili ukumbini, Balozi Maajar
alipata nafasi ya kutembelea meza zote
za maonesho na maelezo na kuchukua
mawasiliano ya wajasiriamali hao, huku
akisisitiza kuwaunganisha katika mtandao
mmoja kupitia ubalozi katika kufanikisha
lengo lao.