Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi,
Amani
Abeid Karume pamoja na mkewe
Mama
Shadya Karume wamepokea zawadi
mbalimbali zikiwemo picha za kuchorwa na
ngao maalumu za heshima, toka kwa
wananchi wa Zanzibar, ikiwa ni shukrani
zao kutokana na mchango wao katika
uongozi.
Waliokabidhi zawadi kwa niaba ya
Wananchi wa Zanzibar ni Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj
Ali Hassan Mwinyi na mkewe Bi. Sitti.
Sherehe zilifanyika katika viwanja vya
Ikulu, Zanzibar.