Tanzania ina idadi kubwa
kiasi gani ya wakazi?
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia takwimu za
mwaka 2008, Tanzania ina wakazi wapatao
milioni 42. Umoja wa Mataifa ulikadiria
mwaka 2009 kuwa Tanzania ilikuwa na
wakazi milioni 43.7.
Watu wangapi wamejiandikisha kupiga kura?
Tume ya uchaguzi ya Tanzania imetangaza
kuwa watu waliojiandikisha kupiga kura
ni milioni 19.
Je
watanzania watapiga kura siku gani?
Siku ya kupiga kura ni tarehe 31 Oktoba
2010
Kampeni zilianza lini na zitaisha lini?
Kampeni za uchaguzi wa Tanzania zilianza
Agosti 31, na mwisho wa kampeni ni
tarehe 30 Oktoba 2010.
Kuna wagombea wangapi wa kiti cha Rais?
Kwa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania kuna wagombea saba, vile
katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar kuna
wagombea sita.
Tanzania ina majimbo mangapi ya uchaguzi?
Kwa Tanzania na Bara na Zanziba kuna
jumla ya majimbo ya ubunge 239
Je
Rais na wabunge hukaa madarakani kwa
miaka mingapi?
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais
huchaguliwa na kuwepo madarakani kwa
muda wa miaka mitano kabla ya uchaguzi
mwingine kufanyika. Sheria hiyo hutumika
kwa wabunge na madiwani.
Jina kamili ni nini?
Nchi hii hutambulika kama Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwa shughuli rasmi.
Je
Tanzania ukubwa wa nchi kiasi gani?
Tanzania ina ukubwa wa kilometa za mraba
945,087.
Lugha Rasmi ni zipi?
Lugha zinazotumika kwa shughuli rasmi ni
Kiingereza na Kiswahili.
Dini kubwa ni zipi?
Ingawa kuna dini nyingine ndogo ndogo,
idadi kubwa ya Watanzania ni Wakristu na
Waislamu.