Imepokewa na Wavuti
Rafiki
yangu (Toninho) ananitumia ujumbe jana akiuliza kuhusu
kufutwa viza ya Tanzania-Afrika Kusini.
Kwa kuwa
sikuwa na majibu kuhusiana na hilo,
niliomba msaada wa majibu toka kwa watu
kadhaa na mojawapo ni katika ukurasa
wangu wa Facebook (marafiki zangu wa
hapo watakuwa wameusoma jana).
Ninamshukuru rafiki yangu kaka Ken wa
kuthibitisha na kuambatanisha nakala (ninayo) ya
barua toka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Tanzania
Investment Center (TIC) akimwandikia
Mwenyekiti wa Kamati ya Watanzania
Botswana kumfahamisha kuhusu kufutwa kwa viza
hiyo.
Sehamu ya
barua hiyo inasema,
"Ninayo
furaha kuwaletea habari njema kwamba
jana tarehe 27 Oktoba 2010, Mhe. Balozi
wa Afrika Kusini na Mkuu wa Kitengo cha
VISA cha Ubalozi huo wamenijulisha rasmi
kwamba kuanzia Novemba Mosi 2010, VISA
kati ya Afrika Kusini na Tanzania
ZIMEFUTWA.
Hizo ni
habari njema za kilio chenu mlichnituma
tulipoonana Mjini Gaborone miezi mitatu
iliyopita."