JK akisalimiana
na mgombea mwenza wake Dk. Mohamed Gharib Bilal
wakati akishuka jukwaani baada ya kumaliza kutoa
salamu kwenye hafla ya kufunga mikutano ya
kampeni kwa CCM iliyofanyika kwenye viwanja wa
Jangwani.

Dk. Mohamed
Gharib Bilal akisalimiana na Rais Mstaaafu wa
awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa na Rais
Mstaafu wa awamu ya pili, Mh. Ali Hassan Mwinyi
wakati alipomaliza kutoa salamu zake kwa wapenzi
na wanachama wa CCM waliofurika katika viwanja
vya Jangwani jijini Dar wakati wa hafla ya
kufunga mikutano ya kampeni.

JK akisalimiana
na wananchi wakati alipowasili kwenye viwanja
vya Jangwani kwa ajili ya kufunga mikutano ya
kampeni kwa CCM.

Sehemu ya
wanachama na wapenzi wa CCM wakiwa wamefurika
katika viwanja vya Jangwani kuhudhuria hafla
hiyo ya kufunga mikutano ya kampeni kwa CCM.

Mgombea wa
Urais kupitia chama cha CUF, Profesa Ibrahim
Lipumba akiwahutubia wananchi wa Manispaa ya
Morogoro kwenye mkutano wake wa kampeni za lala
salama kabla ya kurejea Dar es Saalam kufanya
mkutano wa mwisho wa kufunga kampeni za chama
hicho.

Mmoja wa
shabiki wa Chama cha Wananchi (CUF) akiingia
uwanjani kwa ajili ya kumpokea Mgombea wa Urais
wa Chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba ( hayupo
pichani) siku ya mwisho wa kampeni za uchaguzi
mjini Morogoro kama alivyokutwa.

Baadhi ya
waangalizi wa uchaguzi mkuu wa hapa nchini
kutoka Jumuiya ya Umoja wa Ulaya (EU) ambao
majina yao hayakuweza kupatikana mara moja
walifuatilia mkutano wa kampeni ya mgombea wa
Urais wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ( hayupo
pichani) mjini Morogoro ambao ulikuwa ni kati ya
mikutano yake ya mwisho kabla ya uchaguzi wa
Oktoba 31, mwaka huu.

Mgombea urais
wa CHADEMA Dk. Wilbroad Slaa akihitimisha
mikutano yake ya kampeni jijini Mbeya.

Nyomi ya
CHADEMA katika mkutano huo.

Dk. Slaa
akihutubia umati wa wafuasi wa CHADEMA.

Wagombea uchaguzi
wa Zanzibar. Picha kwa hisani ya Othman Maulid.