Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

 
ProfileToolsGamesCommunity

NEWS

 
 

Dk. Jakaya Mrisho Kikwete atangazwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

05/11/2010

Baada ya siku tano za kusubiri matokeo ya kura zilizopigwa na wananchi siku ya Jumapili, Oktoba 31, 2010 ili kumpata mtu atakayekimiliki kiti cha Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hatimaye matokeo hayo yametolewa na Tume ya Uchaguzi Tanzania, NEC, katika viwanja vya Karimjee jijini Dar Es Salaam. Jakaya Mrisho Kikwete atangazwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuongoza kura asilimia 61.17%.

Habari na Picha

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Jaji Lewis Makame alimkabidhi cheti Mgombea Urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi Dk. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtangaza kushinda katika mbio za urais katika uchaguzi wa mwaka 2010. Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.


Wagombea uchaguzi wa Urais 2010

Matokeo kwa mlinganyo wa kura kwa vyama na wagombezi wake kuanzia kura zilizo chache mpaka mshindi wa uchaguzi wa Urais wa mwaka 2010 ni kama ifuatavyo:

  1. Dovutwa Yahmi Nassoro/UPDP kura 13,176 = 0.15%

  2. Mgahywa Muttamwega Bhatt/TLP kura 17,482 = 0.20%

  3. Rungwe Hashim Spunga/NCCR-Mageuzi kura 26,388  = 0.31%

  4. Kuga Peter Mziray/APPT Maendeleo kura 96,933 = 1.12%

  5. Lipumba Ibrahim Haruna/CUF kura 695,667 = 8.06%

  6. Slaa Willibrod Peter/CHADEMA kura 2,271,941 = 26.34%

  7. Kikwete Jakaya Mrisho/CCM kura 5,276,827= 61.17%

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
News Archive

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©