|
Zenjydar
Community Association, makao yake makuu yapo katika bara la Newham mjini London,
United Kingdom. Tunatoa huduma kwa wahamiaji wa kutoka Tanzania na
wazungumzao Kiswahili wa kutoka Afrika ya Mashariki ambao wanaishi
London na sehemu zingine za United Kingdom. Kwa siku za mbele, tuna
mtazamo wa mipango ya kusaidia nyumbani Tanzania katika mambo madogo
madogo ya kijamii.
Lengo na
madhumuni ya Zenjydar Community Association, ni kuwapatia mafunzo, elimu,
uajira, na muongozo katika mambo ya ustawi wa jamii, uhamiaji,
kuendeleza utamaduni na kujenga umoja wa Watanzania na wazungumzao
Kiswahili wa kutoka Afrika ya Mashariki wanaoishi United
Kingdom, ili tuweze kuendeleza ustadi na kujenga ule ustadi tulionao
katika jamii yetu kwa kuleta maendeleo ya kimaisha ya jamii yetu na
kuchangia katika
kujiendeleza na jamii zingine zilizo hapa Britain.
Zenjydar
Community Association si chama cha siasa na hakitokuwa na msimamo wa
kisiasa wa upande wowote ule. Zenjydar ni 'charity organisation' na
tunaheshimu kila mmoja mwenye mtazamo wake au ushauri wake.
Zenjydar Community Association, is
a not-for-profit organisation based in London Borough of Newham in the
United Kingdom. We provide support to refugees, asylum seekers and
migrants from Tanzania and Swahili speakers from East Africa, who live in
London area and other parts in the United Kingdom. In the near future,
we are looking forward to help to provide basic welfare services back home Tanzania.
Zenjydar Community Association, aims to provide education, training
to improve skills and build capacity, employment, advice
on social welfare, information and guidance for asylum seekers, refugees
and migrants, to promote culture and to bring together Tanzanian community
and Swahili speakers from East Africa who live in London and other parts
in the United Kingdom, to contribute and reach
out in a wider community in British society.
Zenjydar Community
Association, is a charity organisation and is a non-party in politics;
and we respect without distinction of, or any other opinions. |