![]() |
Your community website |
![]() |
||||||
|
|
|
|||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
|
||||||||
|
NEWS archive |
||||||||
|
|
12 August 2007 |
|||||||
Mkutano wa kuanzisha 'forum'
Mwenyekiti wa Zenjydar, aliona ni muhimu kuitisha mkutano huo na kukutana na chama cha EAEF na kufanya mpango wa kukutana na vyama vingine vya Afrika Mashariki, hususan vya ki-Tanzania ambavyo vipo East London ili kujijulisha navyo kikiwa kama ni chama kipya katika vyama vilivyopo na vilevile kupanga mikakati ya kuimarisha umoja wao na huduma kwa jamii ya watu wa nyumbani ambao wanaishi hapa U.K. Zenjydar imeamua kuchapisha mkutano huo kwenye mtandao kwa kuwa tumeona kuna umuhimu wa jamii nzima kujua nini kinachoendelea katika 'Community' yao. Tutawaletea maendeleo ya mikutano yote muhimu pale tutakapoona kuna umuhimu wa jamii kujua kimaendeleo. Mkutano huo ulihudhuriwa na kamati zote mbili wakiwamo: Dk. Mohammed Zahran, Bw. Saleh Jaber, Ust. Khamis, Ust. Khalfan, Bw. Farid na Bw. Said Ahmed. Mkutano ulianza saa tisa kamili juu ya alama. Katibu Mkuu wa EAEF, Dk. Mohammed Zahran, alijitambulisha na akaitambulisha kamati yake ambao waliohudhuria mkutano huo na ambao hawakuhudhuria ambao walikuwa na dharuri ya ghafla. Mwenyekiti wa Zenjydar akachukua fursa ya utambulisho huo na kuitambulisha kamati yake ambao waliohudhuria na ambao hawakuhudhuria ambao walikuwa na dharuri. Mwenyekiti wa Zenjydar alianza kuzungumzia Ajenda ya mkutano huo ambayo (ilizungumzia mambo) matano muhimu. Nayo ni kama ifuatavyo:
1. Kuitambua au kuijulisha Zenjydar: Mwenyekiti aliitambulisha 'organisation' yake kwa kusema ikiwa kama ni 'organisation' mpya ambayo (imezinduliwa rasmi mwezi wa tano mwaka huu 2007, na imeanza kazi zake rasmi mwezi wa saba mwaka huu 2007). Zenjydar si chama cha siasa na hakitokuwa na muelekeo wowote wa kisiasa au mtazamo wa siasa ya upande wowote ule. Na tunaheshimu kila mmoja mwenye mtazamo wake au ushauri wake. Mwenyekiti wa Zenjydar, kaona kuwa kuna umuhimu wa kukutana na 'organisations' zingine za ki-Tanzania na za jamii ya Waswahili, ambazo zipo hapa East London, na kuelezea malengo na madhumuni ya Zenjydar. 2. Lengo na madhumuni ya Zenjydar: Mwenyekiti alieleza kuwa Zenjydar imeundwa kutokana na mahitaji ya watu wetu ambayo yapo wazi katika jamii yetu ambayo mahitaji hayo wengi wetu yamewakwamisha katika kuangalia mustaqbal wao wa kimaisha wakiwemo hapa nchini U.K. Kutokana na hivyo, Zenjydar imetambua mapema kuona kuwa mahitaji hayo kama hayajachukuliwa hatua hivi sasa basi sisi wenyewe na watoto wetu watakuwa katika hali mbaya ya kimaisha, kiuchumi na kimaendeleo katika dunia ya sasa na huko tunapoelekea ikiwa watapata elimu ya kwenda shule au madrasa na kurudi nyumbani bila ya kuwaimarisha na kuwahusisha watoto wetu na mazingira tofauti ya hapa nchini na sisi wenyewe kuwa na umoja wa kufanikisha malengo yetu; kwahivyo watoto wetu watashindwa kujitolea mchango wao wa kielimu na kiuchumi katika jamii yao na jamii ya watu wa kutoka mataifa mbali mbali ambao wana utamaduni tofauti ambao wapo hapa U.K. Mwenyekiti aliendelea na kusema kuwa, takwimu zinaonyesha kuwa, asilimia kubwa ya watoto wetu wa kutoka nyumbani, Tanzania, na wazungumzao Kiswahili wanaotoka Afrika Mashariki, ambao wapo hapa hawafanyi vizuri mashuleni na wanashindwa na watoto ambao wanaotoka mataifa mengine ambao wapo hapa U.K., na wengine baadhi ya vijana wa kwetu hupotea kabisa na kufuata na kukaa na magurupu ya mitaani na kuanza kutumia vitu vya kuwavuruga kiakili vikiwamo (Drugs and Alcohol); sababu moja wapo kubwa ni kuwa baadhi yao hawana nyenzo za kuwafanya waepukane na vitu hivyo angalau baadhi ya wazazi wanajitahidi kuwaongoza watoto wao na kuwapatia nyenzo za kuwawezesha kufikia viwango vya juu kimasomo na kupata uajira wa juu na kushika nafasi za juu katika nchi kubwa kama hii ambayo milango yake iko wazi katika elimu za watoto na vilevile katika elimu za watu wazima. Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa 'Community' na kuwa na umoja wa kufanya kazi pamoja katika kuimarisha jamii nzima ya watu wa kutoka sehemu moja tukiwapo ugenini; lakini kama tutakuwa mbalimbali itasababisha watoto kutokujuana na vilevile itasababisha (social exclusion) au kutengwa katika jamii yako mwenyewe, ni kitu ambacho si sawa kwa yeyote mwenye akili timamu asingependelea jambo hilo limtokee kwake au kwa mwenziwe na yule anayependelea au anashadidia (social exclusion) basi si mtu mzuri yeye mwenyewe na si mtu mzuri katika jamii yake na ni mtu wa kuangaliwa lengo na madhumuni yake. Nyenzo zinaweza kuwa za aina tofauti za kuwafanya vijana wasifikirie mambo machafu na kuwafanya watoke mitaani na magurupu ya kihuni, ni nyenzo ambazo 'Community organisations' zinatakiwa kuifanya kazi hizo kwa jamii yao na jamii ijihusishe katika kuzitumia nyenzo na huduma hizo zinazotolewa na 'organisations' za jamii yao. Vilevile, mahitaji mingine muhimu ni kuendeleza ustadi tulionao, uajira bora, mafunzo ya kupata vyeti vya hapa na kukusaidia na kukuendeleza kimafunzo (kwa mfano: lugha ya Kiingereza tunayoongea juu juu siyo ile utakayofunzwa katika 'Training' ambayo ni fasaha). Kufuatilia mambo ya makazi, mambo ya sheria, mambo ya afya na maendeleo ya kila mtu mwenye ndoto ya kutimiliza kufanya lile zuri analolikusudia katika maisha yake mwenyewe au kujitolea katika kunufaisha jamii nzima. Kwa ufupi, Zenjydar imeundwa ili watu wa nyumbani wapate wepesi wa kuikaribia 'organisation' yao au chombo chao bila ya kuhisi uzito au ukalifishaji. 3. Huduma za Zenjydar: Tangu kuundwa kwake, Zenjydar ina miezi mitatu na ina mwezi mmoja tu tangu ianze kutoa huduma zake mnamo mwezi wa saba mwaka huu 2007. Kamati ya Zenjydar imefanya bidii katika kuipatia jamii yetu huduma tofauti ambazo tunajua kuwa ni za muhimu na zinahitajika. Wachache wameitika mwito wa huduma hizo mpaka sasa na wengi wamo katika kutuuliza vipi wanaweza kuzipata huduma hizo na wengi ambao tumewafahamisha wamegundua umuhimu wa huduma hizi kutokana na mambo yatakavyo badilika kisheria hapa nchini mwaka unaokuja na miaka ya baadaye. Huduma tuzitoazo mpaka sasa zikiwemo:
4. Kushirikiana kwa kuwa na umoja katika kutoa huduma kwa mafanikio ya jamii yetu: Katika mkutano huo, Mwenyekiti alisisitiza ushirikiano baina ya 'organisations' na kuwa na umoja katika kutoa huduma zipatikanazo kwenye kila 'organisation' kwa faida ya jamii yetu na ninaamini 'organisations' zote zimeundwa si kwa ajili ya kushindana au kuwa na faida binafsi au kutafuta umaarufu; bali ni kujitolea kwa kuwa tumepata elimu kidogo hiyo hiyo tulionayo na tumeweza kuchangia katika jamii yetu kuliko kuwa na elimu hiyo hiyo ndogo na usiitumie kabisa katika jamii yako au kwa mtu wako wa karibu huo ni ubinafsi. Alitoa mfano kuwa "hatuwezi wote kuwa wahandisi au (engineers), lazima wengine wawe madaktari na wengine wawe wanasheria na kadhalika". Ikiwa 'organisation' fulani inatoa huduma fulani, basi 'organisation nyingine iwe inatoa huduma zingine ili watu katika jamii yote wapate huduma zote ambazo wanazihitaji wakiwepo hapa nchini; ndio maana ni muhimu kufanya kazi pamoja na kuwa na umoja wa kila 'organisation' kutambua huduma za 'organisation' nyingine ili pale mtu wa kwetu anapohitaji msaada tuweze kumuonyesha njia wapi aende kupata msaada huo ambao anauhitaji. Ni muhimu kutambua kuwa tupo ugenini na ni muhimu kutambua mahitaji makubwa ya watu wetu bila ya kuyadharau na kuyapuuza, kwani ukiangalia ni watu wetu ambao wanaorudi nyuma kimaendeleo kuliko wa jamii zingine huku ugenini na watoto wetu watakulia hivyo hivyo. Mwisho, Mwenyekiti wa Zenjydar alipendekeza katika kamati ya EAEF kuundwa kwa baraza la waswahili waliopo East London, kwa kukutanisha 'organisations' zote kushirikiana katika kutoa huduma zao bila ya kujigawa makundi kwa mafanikio ya jamii yetu na baraza hilo litakuwa linakutana mara tatu au mara nne kila mwaka (yaani kila baada ya miezi mitatu au miezi minne) kuzungumzia maendeleo ya kila 'organisation' na huduma zilizopo za kila 'organisation', ili jamii ipate huduma hizo na wawe na habari mpya kutoka katika 'organisations' zao. Kamati ya EAEF iliikaribisha rai ya kuwa na baraza la umoja na kwa kifupi walizungumzia tena huduma zilizopo katika 'organisation' hiyo na kukubaliana kushirikiana katika kufanya kazi pamoja kwa lengo la kusaidia jamii yetu ikiwa wote tunatoka sehemu moja. Vilevile walipendekeza kuwa tukutane na kamati ya uongozi wa 'organisations' zingine ili tuelezee msimamo wetu huu, ili tufanye kazi pamoja. 5. Mkutano ufuatao: Mwenyekiti wa Zenjydar akamalizia mkutano huo kwa kuahidi kukutana na kamati za uongozi wa 'organisations' zingine (kama watapendelea) na kubadilishana mawazo katika maendeleo ya jamii yetu.
|
||||||||
|
Custom Search
|
||||||||
|
|
|
|||||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
||||||||