Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS archive

 
 

 01 January 2008

Maendeleo ya mikutano ya jumuia za kuanzisha 'forum'

Mahala: 30 Station Road, Manor Park, London, E12

Saa: 9 mchana - 1 usiku

Waliohudhuria:

EAEF: Ustadh Nassor Haroub, Ustadh Khamis Fakih, Moh'd Nassor, Dr. Mohd Z. Salim, Hafidh Karama, Khalfan Abdalla, Abdallah Ali, Mohammed Shaban.

Muzdalifah: Juma H. Juma, Omar Mohammed, Salum Umbaye, Gharib Maalim, Suleiman Hamad. 

Al Noor: Abdallah Said, Mbarak Hussein, Ali Said, Ahmed Masoud, Khelef Mohammed. 

Zenjydar: Saleh Jaber, Farid Nassor.

Ajenda:

  1. Ripoti za Jumuia kwa Mwaka Uliopita (kwa ufupi)
  2. Mipango ya Mwaka Unaokuja
  3. Maeneo ya Mashirikiano
  4. Mengineyo
  5. Tarehe na Mahala pa Mkutano Unaokuja

Ajenda: (1) Ripoti za jumuia (kwa ufupi) (2) Mipango ya Mwaka ujao

Zenjydar:

Madhumuni: Kusaidia jamii katika maeneo ya Uhamiaji, Ustawi wa Jamii, Elimu, Ajira, Mila na Utamaduni.

Matukio:

  • Kushiriki  katika Refugee Week Festival 2007 – Newham
  • Tumehudumia watu zaidi ya kumi na tano kwenye huduma za uhamiaji, elimu, n.k.
  • Kushiriki kwenye mashindano ya mpira wa miguu ya watoto
  • Mashindano ya kusoma Quraan katika mwezi wa Ramadhan 2007
  • Stop and Search workshop
  • Mkutano wa jumuia kuhusu watoto (Anti-social behaviour, Crime and Drugs & alcohol)
  • Sherehe za Eid-el-Adha au Eid-el-hajj

Shughuli zote zilipata mahudhurio mazuri na tunategemea kupata mahudhurio mazuri zaidi katika matukio yajayo ya jumuia.

Ushauri:

  • Kushirikiana katika mambo ya misiba, mikutano na mengineyo katika jamii.
  • Kuboresha mawasiliano ya vyama na jamii kwa njia tofauti.
  • Kuunda mwenendo wa kuendesha 'forum' kabla ya kutoa huduma kwa jamii.

Mipango Ya Baadae:

  • Yalizungumziwa kwa ufupi.

 

Muzdalifa:

Madhumuni: Kuendeleza elimu na kukuza mfuko wa chama.

Matukio:

  • Mikutano miwili ya jumuia mbalimbali hapa UK kuhusu kushirikiana katika mambo ya misiba na maziko.

Mipango Ya Baadae:

  • Yalizungumziwa kwa ufupi.

 

Al Noor:

  • Madrasa ndio shughuli kubwa ya jumuia hii; pia
  • Mradi wa kujenga msikiti
  • Kufanya tafrija za watoto na jamii
  • Mradi wa vifo na maziko
  • Sports

Matukio:

  • Kufanyika kwa tafrija ya michezo huko Northampton na Coventry

Mipango Ya Baadae:

  • Yalizungumziwa kwa ufupi.

 

EAEF:

  • Madhumuni ya jumuia ni kuendeleza elimu ya dunia na elimu ya dini kwa wakazi wa East London.
  • Kusaidia katika shughuli za jamii zinazolingana na Mila na Utamaduni wa watu kutoka Afrika Mashariki.
  • Kushirikiana na Jumuia nyengine nje ya nchi katika kusaidia watumiaji wa huduma hapa UK au huko Afrika ya Mashariki.

Matukio:

  • Mihadhara 2
  • Sala za Idd na taraweh
  • Kuanzisha madrasa hapo Manor Park
  • Jumuia ilisaidia kukusanya zaka na kuzipeleka huko nyumbani wakati wa Idd ya El-Fitri
  • Kusaidia mradi wa Radio kwa jumuia ya Istiqama

Mipango Ya Baadae:

  • Yalizungumziwa kwa ufupi.

 

Ajenda 3. Maeneo ya Mashirikiano:

Mada hii haikuzungumziwa ingawa iligusiwa kwamba maeneo 4 ni muhimu: Elimu, Msikiti, Vifo na Maziko na Vyuo.

 

Ajenda 4. Mengineyo:

Makatibu wakuu wa Jumuia 4 watakuwa ni wawakilishi wa jumuia zao na watakuwa ni kama kamati tendaji itakayoshirikiana na uongozi unaohusika (wanaokabidhi na wanaokabidhiwa) katika kusaidia katika matayarisho ya mikutano ijayo.

Kwa kila kikao jumuia zitakuwa zinabadilishana uongozi (i.e. kutakuwa na 'rotation' ya uongozi baina ya vyama vyote).

Kabla ya kufunga wahudhuria wa kikao wa vyama hivyo walijielezea zaidi masuulia ya kila mtu katika chama chake.

 

Ajenda 5. Tarehe Ya Mkutano Unaokuja:

Tarehe: 03/02/2008. Mahala: Wakering Road, Barking, IG11. Wakati: saa 9 mchana - saa 12 jioni. Mwenyekiti atakuwa: Chama cha Al Noor.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©