Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS archive

 
 

 03 February 2008

Maendeleo ya mikutano ya 'Swahili Forum' East London

Mahala: Wakering Road, Barking, IG11

Saa: 9 mchana - 1 usiku

Waliohudhuria:

Al Noor: Ustadh Ali Nassor, Ustadh Ahmed Mauly, Ustadh Kamal Mohammed, Shk. Ali Said, Ustadh Abdalla Daud, Ustadh Kassim Masoud, Ustadh Hamid Almauly.

EAEF: Dk. Mohammed Zahran, Ustadh Hafidh Karama.

Muzdalifah Leyton: Usatdh Salum Umbaye, Ustadh Gharib, Ustadh Juma.

Zenjydar: Shk. Saleh Jaber

Kikao kilifunguliwa kwa dua na baada ya dua, mwenyekiti wa mkutano huo (Ustadh Ali Nassor) alianza kuzungumzia mada 'minutes' za mkutano uliopita amabazo kopi zake zilisambazwa kwa wanakamati na wajumbe wote waliohudhuria.

Pia akatoa changamoto za vipi jumuia zetu zitaweza kushirikiana katika mada tulizokubaliana kushirikiana katika vikao vya nyuma ambazo zilikuwa ni:

a) Msikiti

b) Madrasah

c) Mazishi au Maziko

Baada ya hapo mwenyekiti akatoa fursa kwa wanakamati na wajumbe waliohudhuria kutoa mawazo yao kuhusu mada (a). Mwenyekiti aliwazungumzia wanakamati waliohudhuria kuzungumzia mada (a); na kufanya utambulisho wa mada (b) na mada (c) katika mkutano huu.

Wanakamati wa jumuia zote waliohudhuria mkutano huo waliunga mkono mada (a) ambayo ni kusimamisha jengo la msikiti na walichangia mbinu na fikra tofauti za kuweza kufikia dhamira hiyo. Ilionekana ni jambo la muhimu sana kulifanya hili jambo kwa pamoja kama alivyotilia mkazo Dk. Mohammed Zahran alipopewa fursa na mwenyekiti; na akaongeza kwa kusema kuwa itasaidia kupunguza kubabaisha jamii. Suala hilo pia liliungwa mkono na viongozi wote waliohudhuria na Ustadh Hafidh Karama aliongezea kusema kuwa tuwape habari jamii vilevile kama inavyoamuliwa kwenye mikutano na isiwe kinyume na yaliyokubaliwa katika vikao vyetu na vilevile kuwe na uwazi katika malengo yetu. Dr. Zahran aliendelea na kuchangia kuwa ziangaliwe njia zingine za kukuza mradi wa msikiti na kwa wale ambao wameshaanza kutoa mchango huo wapewe angalau barua za shukran kwa mchango wao.

Ustadh Gharib (mwenyekiti wa Muzdalifah, Leyton), alipewa fursa na mwenyekiti kuchangia mawazo yake na pia aliunga mkono mada (a) na kuwa wapo tayari kuwa pamoja katika mikakati hii ya makubaliano ya kufanya hili jambo kwa pamoja. Na alisisitiza sana kuhusu mada (b) na mada (c) na kutilia mkazo kuwa mada zote hizi hazina wepesi na zinahitaji ushirikiano wa jumuia zote. Vilevile jambo hilo lilitiliwa mkazo na Ustadh Salum Umbaye wa Muzdalifah, Leyton.

Shk. Saleh Jaber (mwenyekiti wa Zenjydar) aliunga mkono mada (a) na vilevile aliunga mkono yale yaliyozungumzwa na Ustadh Hafidh Karama kuhusu kutoa habari si za kweli kwa jamii au kubabaisha jamii kuwa na habari ambazo sizo zilizokubaliana au sizo zilizozungumzwa katika mikutano yetu, ambazo yeye alitoa rai ya kutungwa 'Policy' au 'Codes of Practice' za kuendesha mikutano yetu ambazo zitasaidia wanakamati au wajumbe wote wawe katika mtiririko mmoja wa kuandaa mikutano kabla ya mkutano, tunapokuwa mkutanoni na nini la kufanyika baada ya mkutano, angalau kila jumuia ina 'Policy' zake za kuendesha mikutano, n.k., lakini ni muhimu kuandaa 'Policy' ya forum au umoja wa jumuia zetu. Kwa kusisitiza huko, ni yale yale aliyoyazungumzia katika mikutano iliyopita ukiwamo mkutano wa tarehe 01/01/2008. Zenjydar ikajitolea kuzitayarisha 'Codes of Practice' hizo na kuahidi kuzitoa rasmi katika mkutano ujao na kuzituma kwa upendekezo kwa njia ya barua pepe kabla ya mkutano huo ambao Zenjydar itakuwa kama mwenyekiti wa mkutano huo.

Vilevile mwenyekiti wa Zenjydar alichangia kusema ni muhimu kuitisha mkutano wa Waswahili ili kuwatambulisha nia na dhamira ya mada hizo na nini tunataka kufanya katika jamii yetu, ambao mkutano huo utasaidia kuonyesha kuwa hakuna mpasuko wa kijamii katika jumuia zetu na sote ni wamoja. Vilevile aliunga mkono rai ya Dk. Mohammed kutafuta njia zingine za kukuza mradi wa msikiti iwapo hakuna uwezekano wa kupata msaada huo kutoka kwenye vyombo vya mamlaka.

Shk. Ali Said wa Alnoor alizungumzia kuhusu mradi wa msikiti na alizungumzia kuhusu walipofikia katika kutafuta jengo maeneo ya Barking au Dagenham kama walivyozungumzia jumuia zingine zote pamoja na jamii siku za nyuma.

Mkutano uliendelea na kuleta mjadala mkubwa juu ya sehemu ya jengo la Msikiti na Uongozi. Katika mjadala huo, kamati ilileta hoja ya kuwa vipi iwapo eneo litapatikana jirani ya Barking & Dagenham, mfano Newham au Waltham Forest au Redbridge, n.k.

Kutokana na mjadala huo ambao ulionyesha kuna hoja ya mambo mengi yatahitaji mabadiliko katika kulifanya hili jambo kwa pamoja, viongozi wa Zenjydar, EAEF na Muzdalifah waliona kuwa kuna umuhimu wa kuleta sera au 'Policy' za mradi wa msikiti ili tuangalie sehemu gani zinaweza zikafanyiwa marekebisho ya kuweza kulifanya hili jambo kwa pamoja.

Ikashauriwa kuwa Alnoor watume 'Policy' kwa jumuia zingine ili zipitiwe na jumuia zingine kabla ya mkutano ujao ambao utakuwa tarehe 02/03/2008 na kuangaliwa vipi tunaweza kuirekebisha ili tukubaliane kwenye maeneo ya Uongozi na maeneo ya ujenzi wa Msikiti.

Kabla ya mkutano kumalizwa, yaliongezewa yale ya mada (b) na mada (c) ambayo kila jumuia iliombwa mambo maalum kuchangia vipi tunaweza ku 'implement' mambo hayo kwa pamoja katika jamii na kwa faida ya jamii.

Mkutano ujao ni tarehe 02/03/2008, Manor Park, E12 - Mwenyekiti wa mkutano huo ni jumuia ya Zenjydar Community Association.

Angalia ajenda ya mkutano ujao wa tarehe 02/03/2008 hapo chini.


TAREHE: 02 Machi 2008

SAA: 9 mchana – 1 usiku

MAHALI: Manor Park, E12

Walioalikwa:

Muzdalifah, East African Education Foundation, Alnoor, Zenjydar Community Association

 AJENDA

 1. Ufunguzi wa Mwenyekiti

- Utambulisho wa kamati

- Mkutano uliyopita na ‘misunderstanding’ iliyojitokeza

 2. Maoni kuhusu MAZISHI kama yalivyoombwa katika mkutano uliopita:

- Alnoor

- EAEF

- Muzdalifah

- Zenjydar

 3. Kuirejea sera ya mradi wa msikiti: 

- Vipengele vya makubaliano (EAEF, Muzdalifah, Zenjydar)

- Vipengele vya mapingano (EAEF, Muzdalifah, Zenjydar)

- Mjadala

- Matokeo katika:

o       (vipengele vya makubaliano)

o       (vipengele vilivyopingana)

5. Mengineyo

6. Mkutano ujao

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©