Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

NEWS archive

 
 

 02 March 2008

Maendeleo ya mikutano ya 'Swahili Forum' East London

Mahala: Manor Park, E12, Newham, London

Saa: 9 mchana - 1 usiku

Waliohudhuria:

Al Noor: Ustadh Ali Nassor, Ustadh Mbarak Hussein, Ustadh Sabry, Ustadh Said Mohammed, Ustadh Said, Ustadh Ali Said.

EAEF: Ust. Khalfan, Ust. Khamis Faki, Dk. Mohammed Salim, Ust. Hafidh Karama, Ust. Nassor Haroub.

Muzdalifah Leyton: Ust. Khalfan, Ust. Khamis Faki, Dk. Mohammed Salim, Ust. Hafidh Karama, Ust. Nassor Haroub.

Zenjydar: Shk. Saleh Jaber, Shk. Farid Nassor

1. Mkutano uliyopita na mambo yaliyojitokeza ambayo yanahitaji uamuzi wa kamati ya ‘forum.

  1. Jina la ‘forum’: Imejitokeza kuwa bado halijapatikana jina kamili la umoja wa jumuia husika kutambulika kijina katika jamii na katika vyombo tofauti (tunataraji katika mkutano ujao kutatafutiwa muda mchache wa kupiga kura ya jina la umoja wa jumuia husika).

  2. 'Codes of practice': Zenjydar wametoa 'codes of practice' kwa jumuia zote kama ilivyoombwa katika mkutano uliopita na ikaomba kila jumuia kuchangia mawazo ili ziweze kulingana na mwenendo wa umoja wa jumuia husika.

2.      Maoni kuhusu maziko na matokeo yake: 

-          Jumuia zote zimeunga mkono jambo la maziko. 

-          Jumuia zote zimekubaliana kuwa na mfuko mmoja (mfuko mama). 

-          Jumia zote zimekubaliana kuwa na kamati moja ya kutekeleza utendaji.

Baada ya matokea hayo, jumuia zimeamua kuzungumzia vitu ambavyo vinahitaji wasaa mrefu katika ajenda ya mikutano ijayo vinavyohusu maziko ambavyo havijafikia uamuzi. 

3.      Kuirejea sera ya ‘The Masjid Project’:

Vipengele vya sera ya ‘The Masjid Project’ vilipitiwa na jumuia zote na matokeo hayajafikia mwisho au ‘conclusion’. Ama baada ya mjadala mrefu, imeelekea kuwa mjadala huo umeleta chimbuko la uamuzi wa mwisho wa maelewano ya jumuia zote kufikia uamuzi wa kupendeza kwa kila jumuia husika katika ‘The Masjid Project’ na vilevile kuendelea na malengo na mikakati mingine kwa pamoja ambayo yenye kuleta maendeleo katika jamii yetu. 

4.      Mengineyo:

1.   Kuzidisha ‘exchange of communication’ habari tofauti kati ya jumuia nne na jamii.

2.   ‘Codes of Practice’ ziwe ‘practiced’. 

5.      Mkutano ujao: 

Tarehe 06/04/2008, Jumapili, saa 9 mchana – saa 1 usiku. Manor Park, E12. Mwenyekiti wa mkutano ni jumuia ya Muzdalifah.

 

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©