|
|
|
|
|||||
|
|
|
||||||
|
|
|||||||
|
|
|||||||
|
Ramadhan Qur'an Contest 2008 - 20/09/2008 |
|||||||
|
|
|||||||
|
Mashindano ya pili ya Qur'an (Ramadhan Quran Contest 2008) ambayo yamefanyika tarehe 20/09/2008 yamekuwa ya mafanikio makubwa kama alivyosema Mwenyekiti wa Zenjydar Community Association bwana Saleh Jaber. Mashindano ya mwaka huu kulinganisha na ya mwaka jana, imeonyesha kuwa na maendeleoa katika mashindano hayo ambayo yameshukuriwa na kamati ya Zenjydar kwa wote waliochangia kufanya mashindano hayo kufanyika. Mwaka huu Zenjydar imealika vyuo vyote kushirikisha watoto wao katika mashindano hayo tangu mwezi wa nne (April 2008) ambayo matokeo yake baadhi ya vyuo vimeshiriki na baadhi ya vyuo vimekutwa na dharura ya kutokushiriki. Vilevile mwaka huu, Zenjydar imetanua mualiko wake wa watoto kushiriki katika mashindano hayo kwa kuwakaribisha wazazi na familia mbalimbali kujisajili na kushiriki katika mashindano hayo na Zenjydar inashukuru jitihada za Waalimu na Wazazi wote ambao wameshiriki na kuwabiidisha watoto wao kushiriki katika mashindano hayo katika mwezi mtukufu wa Ramadhan. Vilevile, shukran kwa wote waliorudisha fomu za mawazo ambazo zilitolewa na Zenjydar kwa jamii ili kufanikisha jambo hili. Mwenyekiti wa Zenjydar, bwana Saleh Jaber alisema katika mashindano hayo kuwa, kuwashirikisha na kuwapa watoto fursa ya kuja kuwashirikisha katika mashindano haya yanasaidia watoto na walimu pamoja na wazee kujua maeneo gani watoto wanahitaji kuendelezwa zaidi katika kuisoma Qur'an kwasababu ya makosa madogo madogo yanayotolewa na majaji wanaoaminika wa mashindano hayo. Na zaidi mtoto atakavyoshiriki katika mashindano ndio zaidi anakuwa imara katika kuisoma vizuri Qur'an. Mashindano ya mwaka huu kulikuwa na majaji watatu: Ust. Sabry (aliangali Hukmu ambazo ndio kitovu cha Qur'an). (الاظهار ,الادغام ,الاقلاب ,الاخفاء ,ميم ساكنة , قلقلة , Ra رَ , Ri رِ , na Shaddah) Washindi wa mwaka huu ni kama ifuatavyo: - Mshindi wa kwanza - Rahma Mohammed - Mshindi wa pili - Omar Salim - Mshindi wa tatu - Ahmed Salim - Shahada ya Sauti nzuri - Munawwar Mussa - Shahada ya Lafdhi nzuri - Omar Salim - Shahada ya 'Confidence' - Rahma Mohammed - Shahada ya 'Appearance' - Rahma Mohammed
(Kwa maelezo zaidi kuhusu mashindano ya Ramadhan Qur'an Contest wasiliana na bwana Farid Nassor 07951483375 au Saleh Jaber 07886535282)
|
|||||||
|
Custom Search |
|||||||
|
|
|
|
|||||
|
©
www.zenjydar.co.uk - Since 2007 |
|
|||||||