Mount Kilimanjaro

 

 

 

Your community website

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

Meetings & Agendas

 

Fatilia mikutano inayohusu jumuia yako kwa kuangalia vichwa vya habari na kubonyeza kwenye picha ya kitabu na kalamu iliyopo chini

Tunajaribu kuwaletea ajenda na ripoti ya mikutano yote inayotokea katika kuleta maendeleo ya jumuia yetu. Sababu ya kufanya hivi ni kuifanya jamii ijue kila chama katika jumuia yao nini kinafanya, na katika umoja wetu wa kuleta maendeleo ya jamii wapi tumefikia.

Tutumie rai zako katika email ya zenjydar@gmail.com kama una mtazamo wowote tofauti na ajenda zetu za kuleta maendeleo ya jamii yetu.

Baada ya mkutano wa tarehe 12/08/2007 baina ya Zenjydar na East African Education Foundation juu ya kuanzisha 'forum' ya vyama vya Waswahili wa Tanzania, East London. Mkutano mwingine uliitishwa na Zenjydar Community Association katika mwezi wa Disemba 2007 ambao uliwaalika East African Education Foundation na Alnoor CET. Kutokana na mambo mengi yamekabili vyama hivi katika kufikia mwishoni mwa mwaka na sherehe za Eid-el-hajj, mkutano uliamuliwa ughairishwe na kufikiriwa kufanywa siku za baadaye.

Mpaka sasa, vyama ambavyo vimeonyesha dalili nzuri juu ya fikra hiyo ya kuwa kitu kimoja na kuleta maendeleo hayo katika jamii ni: Zenjydar Community Association, East African Education Foundation, Muzdalifah na Alnoor CET.

Vyama hivi vitakutana kila baada ya miezi kadhaa kama itakavyoamuliwa katika mikutano ijayo na kuzungumzia mikakati na mbinu za kuleta maendeleo. Imeamuliwa kuwa kila tutakapokutana chama kimoja wapo kati ya hivyo kitashika kiti cha mkutano na mambo ya uongozi wa ajenda, kutayarisha ripoti ya mkutano, mawasiliano baada ya mkutano mpaka mkutano ujao ambao chama hicho kitakabidhi kiti hicho na masuulia hayo kwa chama kingine na kuendelea na mzunguko huo kwa vyama vingine husika kwenye kila mikutano ijayo.

Vyama hivyo vimeona hakuna budi ya kupoteza muda bali kuanza na mikutano ya kuanzisha umoja huo wa kuleta maendeleo. Mkutano wa tarehe 01/01/2008 ambao ulifanyika Manor Park, ulisimamiwa na kushikwa kiti chake na East African Education Foundation na mikutano ifuatayo itashikwa viti na jumuia zingine kama duru.

Kila chama kitakuwa kinafanya kazi zake 'projects' tofauti binafsi ila vitakapokutana vitazungumza maendeleo ya waliyoyafanya katika 'projects' zao na kufuma mbinu mpya za 'forum' katika kusaidia jumii.

 

02/03/2008

Maendeleo ya mikutano ya 'Swahili Forum' East London, ya kuleta maendeleo ya kijamii ya Waswahili. Vyama vinavyoshiriki katika maendeleo hayo ni: Zenjydar Community Association, East African Education Foundation, Muzdalifah na Alnoor.

 

03/02/2008

Maendeleo ya mikutano ya 'Swahili Forum' East London, ya kuleta maendeleo ya kijamii ya Waswahili. Vyama vinavyoshiriki katika maendeleo hayo ni: Zenjydar Community Association, East African Education Foundation, Muzdalifah na Alnoor.

 

01/01/2008

Maendeleo ya mkutano wa kuanzisha baraza (forum) ya Waswahili wa East London. Vyama vinavyoshiriki katika maendeleo hayo ni: Zenjydar Community Association, East African Education Foundation, Muzdalifah na Alnoor CET.

 

12/08/2007

Mkutano baina ya Zenjydar na East African Education Foundation juu ya kuanzisha baraza (forum) ya Waswahili, East London, katika juhudi ya kuleta umoja na maendeleo.

 
 

 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©