Mount Kilimanjaro

Beit El Ajaib
     

HomeNewsServicesEventsAbout UsContact Us

ProfileToolsGamesCommunity

YOUR VOTE YOUR FUTURE

 

MASWALI NA MAJIBU YA KUPIGA KURA NCHINI UK:

Suali:

Je, ninatakiwa kujisajili kwa kupiga kura kila mwaka au mara moja tu?

Jibu:

Unatakiwa kujisajili kila mwaka kati ya mwezi wa nane (Agosti) mpaka mwezi wa kumi na moja (Novemba). Fomu za kujisajili kwa kupiga kura hujulikana kama "Annual Canvass" hutumwa kwako kwa njia ya posta kutoka katika baraza la Upigaji Kura.

Kujisajili kwa kupiga kura katika nyakati nyingine za mwaka, bonyeza kwenye kiungo hapa kwa fomu mpya.

Suali:

Je, maelezo yangu binafsi ninayojaza katika fomu ya usajili wa kupiga kura yanaonekana na sekta nyingine au (third party)?

Jibu:

Kuna nakala mbili za kujisajili na kupiga kura (katika fomu yako). Kuna "The full version" na "The edited version".

Hata kama unatumia anuani mbali, ukichagua "The full version", jina lako litatumika kwa upigaji kura na vilevile linakusaidia kupata mikopo mikubwa katika mabenki, kwani mabenki hutumia Electoral Register kufanya Credit Check yako kwa kukupatia mikopo mikubwa.

Ukichagua "The edited version" katika fomu, unaweza kuchagua aidha jina lako litokee na anuani yako kwa madhumuni ya kupiga kura tu, au bila ya anuani yako. Kwenye "The edited version", jina lako linaweza kutumika na sekta nyingine za kibiashara kukutumia matangazo mbalimbali ya kibiashara.

Suali:

Je, nitajuaje kama jina langu limeshaandikishwa kwa kupiga kura?

Jibu:

Kama umejaza fomu na kuituma fomu ambayo imeletwa kwako kwa njia ya posta kati ya Agosti na Novemba 2007, jina lako litakuwa limeshaandikishwa kwa kupiga kura.

Kama umehamisha anuani kati ya Disemba na Septemba unatakiwa kujiandikisha tena kwa kupata fomu mpya kwa njia ya mtandao kwa kubonyeza hapa.

Hauwezi kujisajili kwa njia ya simu, lakini unaweza kuwapigia simu Electoral Register yako wakutumie fomu mpya.

Suali:

Je, Kwanini natakiwa kujisajili kwa kupiga kura?

Jibu:

Unatakiwa uwe katika Electoral Register kwa kupiga kura nchini UK na hausajiliwi 'automatically' ni lazima ujaze fomu.

Ukitumiwa fomu ni lazima uirudishe kwa Electoral Register au watakuchaji faini ya £1000 vilevile kama hujisajili hakusaidii Credit Rating yako ambayo inakusaidia katika mipango ya kifedha na mabenki.

Suali:

Nani anaweza kujisajili na Electoral Register?

Jibu:

- Yeyote mwenye miaka 16 au zaidi (lakini huwezi kupiga kura mpaka ufike miaka 18).

- Raia wa UK, Republic of Ireland na raia wa nchi za umoja wa madola (Commonwealth) ambaye ana sheria ya kuishi hapa nchini UK.

- Raia wa nchi za Ulaya (EU) ambaye anaishi UK, raia wa Channel Islands, Isle of Man, na raia wa miliki za nchi za British ambaye anaishi UK.

Nchi za umoja wa Ulaya (European Union)

Austria
Belgium
Bulgaria
Cyprus
Czech Republic
Denmark
Estonia
Finland
France
Germany
Greece
Hungary
Ireland
Italy
Latvia
Lithuania
Luxemburg
Malta
Netherlands
Poland
Portugal
Romania
Slovakia
Slovenia
Spain
Sweden
United Kingdom

 

Nchi za umoja wa madola (Commonwealth)

Antigua and Barbuda
Australia
The Bahamas
Bangladesh
Barbados
Belize
Botswana
Brunei Darussalam
Cameroon
Canada
Cyprus
Dominica
Fiji Islands
The Gambia
Ghana
Grenada
Guyana
India
Jamaica
Kenya
Kiribati
Lesotho
Malawi
Malaysia
Maldives
Malta
Mauritius
Mozambique
Namibia
Nauru
New Zealand
Nigeria
Pakistan
Papua New Guinea
St Kitts & Nevis
St Lucia
St Vincent & The Grenadines
Samoa
Seychelles
Sierra Leone
Singapore
Solomon Islands
South Africa
Sri Lanka
Swaziland
United Republic of Tanzania
Tonga
Trinidad & Tobago
Tuvalu
Uganda
United Kingdom
Vanuatu
Zambia
Zimbabwe

 

Kwa maswali na majibu yote kuhusu kupiga kura bonyeza hapa

   
 

Custom Search

Go up

 

Quick Links

Watch Television
Events Calendar
News Archive 2008
News Archive 2007

External Links

Alnoor CET
TZ Embassy UK
TZ's Community UK

© www.zenjydar.co.uk - Since 2007 | Web master | Site map | www.zenjydar.co.uk - Since 2007 ©