Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 04/08/2007

CLOUDS MEDIA YACHUKUA KOMBE LA RAHA

__________

__________

__________

__________

Timu ya Clouds Media iliyopo Dar es Salaam, imejichukulia kombe la kugombea mshindi wa kombe la Raha la mwaka 2007. Pichani juu, Kepteni wa timu hiyo Kepteni Shafii akinyanyua kombe la ushindi la Raha la mwaka 2007, katika fainali ya kombe hilo. Clouds Media ambayo imemshinda mpinzani wake Raha katika fainali hiyo kwa mabao 3-2. Katika purukushani za kugombea kombe hilo, golikipa wa timu ya Raha alipoteza fahamu baada ya kugongana na mchezaji mwenzake. Golikipa huyo alipata huduma ya kwanza hapo hapo uwanjani na baadaye akachukuliwa kupelekwa hospitali na hakuchukuwa muda mrefu kurudi hali yake ya kawaida.


NDEGE YATUA KICHWA-KICHWA

Ndege ya Precision Air, ambayo inamilikiwa na shirika binafsi la Precision Air ya Tanzania, ilitua kidharura wakati wa safari yake kutoka Zanzibar kwenda Nairobi. Ndege hiyo ilipata matatizo ikiwapo hewani, lakini rubani wake alijitahidi kuitulisha ndege hiyo kidharura  na kusababisha kuvunjika tairi lake la mbele. Bahati, hakuna mtu aliyejeruhiwa vibaya.


TAREHE 05/08/2007

WATANZANIA WA MAREKANI

Wa Tanzania

__________

Wa Kenya

__________

Wa Eritrea

Timu ya Watanzania wa Marekani wamejipatia nafasi ya pili katika kugombea kombe baada ya kushindana na timu ya Kenya na Eritrea waliopo mjini Atlanta, Marekani. Watanzania waliishinda timu ya Eritrea mabao 2-0, na kufungwa na timu ya Kenya mabao 2-1, katika fainali.


TAREHE 06/08/2007

SAMORA AVENUE - DAR ES SALAAM

Jengo la Mtaa wa Samora Avenue, Dar es Salaam, ambalo linavunjwa ili kujengwa jengo lake jipya

__________

Baadhi ya wapangaji wakilalamika uvunjaji wa jengo hilo

__________

Daraja la Manzese, Dar es Salaam, hivi sasa


TAREHE 07/08/2007

UTAWALA WA UCHINA

__________

__________

__________

Masanamu haya ambayo yapo China, yalikuja kuonekana mwaka 1974 na Mkulima aliyopo China, Bwana Yang wakati alipokuwa akichimba kisima uwani mwa nyumbani kwake na kukuta yamefukiwa ardhini zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Masanamu hayo ambayo idadi yake ni zaidi ya 7000 (elfu saba) wakiwamo masanamu ya mafarasi, yana umri zaidi ya miaka 2200 (elfu mbili mia mbili) tangu kutengenezwa kwao na kuchimbiwa chini ya ardhi.

Masanamu hayo ambayo yana kimo cha mtu yalizikwa pamoja na mfalme wa kwanza wa China wa wakati huo, mfalme Qin Shihuang. Madhumuni ya kuchongwa na kuzikwa pamoja na mfalme huyo ni kuwa, mfalme Qin alikuwa ana khofu kubwa sana ya kifo chake na alitaka kuendelea utawala na kuendeleza ufalme wake baada ya kufa kwake, ndio maana alitoa amri ya kuwatengeneza mafuasi hao pamoja na farasi zake kwa kutegemea kuwa watamsaidia baada ya kufa kwake katika maisha yake ya pili. Kila fuasi mmoja ana sura tofauti na mwenzie, na kila mmoja alizikwa na silaha tofauti zikiwamo mapanga, majambia na mishale ya kweli na yenye thamani kubwa, ambazo silaha hizo zinasemekana ziliibiwa baada tu ya kuzikwa kwa mfalme huyo zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita.

Baadhi ya masanamu hayo yameshachimbuliwa kwenye ardhi na wamehifadhiwa sehemu maalum. Kati ya masanamu 7000, masanamu 120 (mia moja ishirini) watachukuliwa kutoka China na kuletwa London kwa maonyesho maalum katika makumbusho yaliyokuwepo mjini London. Maonyesho hayo yataanza tarehe 13/09/2007, katika makumbusho ya London.


TAREHE 08/08/2007

GATINI - DAR ES SALAAM

Hili ndio Gati la boti ziendazo Zenjy kutoka Dar, kama lionekanavyo hivi sasa.

__________

TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Huu ni ustadi wa wana teknolojia ambao wamebuni nguo hiyo hapo juu pichani ambayo ina kiti cha kukalia. Kiti hiko ambacho kimeunganishwa na nguo ambayo kila hatua unayotembea inajaza hewa kwenye kiti kupitia mpira maalum ambao umeunganishwa na kiatu chake.

__________

OLIMPIK 2008 - CHINA

__________

__________

__________

Wachina milioni moja wameshiriki katika kusheherekea siku za mwisho mwisho zinazoelekea katika sherehe kubwa za Olimpik mwaka 2008, ambazo zitafanyika huko huko China. Baraza la olimpik la uchina limesema kuwa Olimpik hiyo itawaletea michezo na sherehe ambazo hazijawahi kutokea.


TAREHE 09/08/2007

MTU MREFU DUNIANI

__________

__________

__________

__________

Leonid Stadnyk ni mtu mrefu duniani ambaye kamshinda mpinzani wake mchina Bwana Bao Xishun kwa urefu wa kichwa tu. Leonid anaishi nchini Ukraine katika kijiji cha Zhytomyr. Bwana Leonid ana urefu wa futi 8 na inchi 11 karibu futi 9, na anavaa viatu saizi inchi 17. Katika vipimo vya mwaka 2004, Bwana Leonid alikuwa na urefu wa futi 8 na inchi 4, kwahiyo kaongezeka kwa inchi 7 kwa muda wa miaka mitatu, inasemekana bado anaendelea kukua. Juzi-juzi, Bwana Leonid alizawadiwa zawadi ya viatu na mtengenezaji viatu maarufu wa Ujerumani, Bwana Georg Wessels.


TAREHE 10/08/2007

THE GREAT WESTMINSTER CLOCK

Hapo juu ni picha za saa maarufu ya London, (The Great Westminster Clock) ambayo kwa wengi wanaijua kwa jina la Big Ben. Saa hiyo ilitengenezwa na Bwana Edward Dent na ikaanza kazi yake mwaka 1859, na tangu imeanza kufanya kazi, haijawahi kusimama hata siku moja. Mnara huo wa saa ambao umenyanyuka juu ya qasri la Westminster, umepata umaarufu wa Big Ben, lakini Big Ben si jina la mnara huo kama wengi wajuavyo. Big Ben ni jina la kengele ambayo imo ndani ya mnara huo ambayo kazi yake ni kugonga kengele kila ifikapo saa kamili katika kila saa.

Mtambo wa saa hiyo, upo kwenye chumba maalum cha chini ya saa yenyewe ambao umakaniki wake unaangaliwa na watu maalum watatu. Mwaka 2009 (The Great Clock) itasheherekea kutimiza miaka 150 tangu ianze kazi yake. Tarehe 11/08/2007, ndio siku ya mwisho saa hiyo kusikika kugonga kwa sauti yake kila ifikapo saa kamili, kwasababu ya matengenezo ya kengele yake (Big Ben) mpaka mwezi wa tisa (September) mwaka huu 2007, mpaka itakapoanza tena upya, lakini saa itaendelea kufanya kazi kama kawaida. Kazi hizo za matengenezo zitafanyika kwenye mtambo wake wa saa hiyo tu na usafishaji wa vioo!

Big Ben, ambayo ni jina la kengele tu, na si mnara wa saa, ina uzito wa tani 13.5. Nyundo inayogongea kengele hiyo ina uzito wa kilo 200. Mnara huo wa saa ambao una pembe nne, una maduara manne ya uso wa saa zake. Kila duara moja limejengwa kwenye kila upande mmoja wa mnara huo. Duara moja la uso wa saa hiyo una kipenyo cha mita 7 au (diameter), ambayo kila duara la saa hizo zimejengewa na vipande vya vioo 312 vya madini ya (opal) katika duara moja. Na kila duara moja linamulikwa na balbu 28 za taa ambazo zinadumu kwa masaa 66,000 (elfu sitini na sita) kuanzia upya wake.

Mnara wa saa au (clock tower) una urefu wa mita 96, na ngazi 292 kuanzia usawa wa bahari mpaka chumba cha saa yenyewe, na ziada ya ngazi 101 kuanzia kwenye chumba hicho mpaka chumba cha kileleni.

- Picha za mnara wa saa na Phil Coomes -


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk