Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 21/07/2007

MAFURIKO - UNITED KINGDOM

Wakala wa mazingira wa U.K. wametoa onyo kali la mafuriko katika bara la Midlands (bara lililopo katikati ya U.K.) ambalo mito yake mikuu (Avon, Severn, Dene, Isbourne, Stour na Teme) yalifurika maji kupita kiasi.

Pia wameonya wakala hao ya kuwa, baadhi ya maeneo ya Oxfordshire, Berkshire na London, kuna uwezekano wa kunyesha mvua hizo katika siku zijazo. Onyo hilo lilitolewa baada ya sehemu mbalimbali za U.K. kunyeshewa mvua ya miezi miwili kwa muda wa siku moja na kusababisha mafuriko ya maji ambayo yameathiri usafiri na makazi ya wananchi.

Waziri Mkuu wa U.K., Bwana Gordon Brown ametamka, mafunzo yamesomwa katika mafuriko yaliyotokea na amesema hatua zaidi zinachukuliwa za kukadiria vipi usafiri na mifereji ya kupitishia maji yaweze kupokea dharura kama hii ambayo si ya kutegemewa iwapo itatokea tena hapo baadaye. Amewasisitiza wakala wa mazingira na wakala wa usafiri kushirikiana zaidi katika kazi zao ili kupunguza athari za maisha ya watu na kazi zao za kila siku. Vile vile amezipongeza huduma za dharura na wanajeshi waokovu kwa kazi nzuri walioifanya katika uokovu wa watu kwenye mafuriko.

__________

MATENGENEZO YA UWANJA WA KARUME

__________

__________

Ukarabati wa Uwanja wa Karume ukiwa njiani. Uwanja huo utafanyiwa kuwa ni kituo cha taifa cha soka cha timu za kimataifa na timu za vijana na watoto wa nyumbani kufanya mazoezi yao na kuweka kambi.

__________

NGOMA YA PUNGWA

Sherehe za ufunguzi wa Tamasha la Mzanzibari zilizofanyika huko Uroa, mkoa wa kusini Unguja, ambako sherehe za mwaka kogwa hufanyika kila mwaka. Hapo juu ni kikundi cha utamaduni wakicheza ngoma ya Pungwa.

__________

TAREHE 22/07/2007

KUPIMA KWA HIYARI

Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Lowasa akijitolea kupima ugonjwa wa ukimwi yeye na mkewe katika kampeni ya kupima kwa hiyari.

__________

TAREHE 23/07/2007

MWAKA KOGWA - ZANZIBAR

Mfagia njia

__________

Vita vya bakora za majani ya mgomba

__________

Leo kazi ipo!

__________

TAREHE 24/07/2007

BILL CLINTON NA JAKAYA KIKWETE - TANZANIA

__________

TAREHE 25/07/2007

NAULI YA DALADALA IMEPANDA JUU

Nauli ya daladala na nauli za mabasi ya kwenda mikoani zimepanda kuanzia tarehe 25/07/2007.

__________

TAREHE 26/07/2007

TIMU YA VIJANA WA UMRI WA CHINI YA MIAKA 17 YA ZANZIBAR

__________

__________

Timu ya vijana wa umri wa chini ya miaka 17 ya Zanzibar, wakiwa wakijichana na misosi huko mjini Cairo katika ziara ya wiki mbili ya kupiga kambi na kocha wa timu wa kutoka Egypt. Vijana walirudi majuzi ambapo walikuwa katika kambi hiyo wakijitayarisha na kombe la vijana la Afrika mashariki na kati ambalo limedhaminiwa na Rais wa Rwanda, Bwana Pierre Nkurunzinza na kombe limetayarishwa na kutolewa na Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete. Kila la kheri vijana wetu.

__________

LIVERPOOL F.C. WAZINDUA PLAN YA UWANJA MPYA

__________

Liverpool F.C. wamezindua plan ya uwanja wao mpya ambao wanategemea kuanza ujenzi huo hivi karibuni. Uwanja huo ambao una viti elfu sitini, utagharamia £300 milioni (paundi milioni mia tatu za U.K.) na unategemewa kuisha ujenzi wake mwaka 2010.

__________

Washabik wa Liverpool F.C., Dar-es-Salaam

__________

Tumepitwa na sabasaba mwaka huu.

__________

TAREHE 27/07/2007

ZIARA YA BILL CLINTON - TANZANIA

__________

__________

Rais wa 42 wa Marekani, Bwana Bill Clinton alikuwa katika ziara ya siku chache nchini Tanzania katika kampeni yake ya kupigana vita na maradhi ya Malaria na Ukimwi ambayo yanauwa wengi nchini Tanzania na nchi nyingine za Afrika. Ex Rais Clinton amefungua kampeni hiyo ambayo ameipa jina la CHAI (Clinton Foundation for HIV/AIDS).

- Picha na Issa Michuzi - Asante Kaka!

© www.zenjydar.co.uk