Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 28/07/2007

MAFURIKO - CHINA

Mafuriko yaliyoikumba China katika mji wa Wuhan, ambayo mafuriko hayo yalisababisha kuathiri baadhi ya barabara na nyumba ambazo zimewaacha watu milioni 119 kuathirika na mafuriko hayo. Gharama za mafuriko zimekadiriwa kufikia £3 billion (bilion tatu za U.K.) mpaka hivi sasa na huku wataalamu wa hali ya hewa wa China wanatarajia kupata mvua zingine za nguvu katika siku zijazo. Red Cross waliopo China wametangaza kwa kupitia kwa waandishi wa habari kuwa, watu 650 wamefariki kutokana na mafuriko hayo. Wakati huohuo mjini Kathmandu, Nepal, jirani na Uchina, wamepatwa na mafuriko hayo na yameua watu 71,000 (sabini na moja elfu) na kuwacha maelfu bila ya makazi. Mafuriko hayo yamefika mpaka Kaskazini mwa Bangladesh, ambayo pia yameacha baadhi ya watu bila ya makazi.

__________

MAFURIKO - BANGLADESH

__________

MTOTO WA SHULE - INDIA

Mtoto wa shule akivuka daraja kuwahi nyumbani baada ya kumaliza masomo yake huko mjini Dass, India. Mji huo ni mji wa pili duniani kwa ubaridi, ambao hali yake ya ubaridi wa chini kabisa ni (-60°) ambayo ilirekodiwa na vipima joto mwaka 1995.


TAREHE 29/07/2007

MAONYESHO YA MASHINDANO YA MANUVA YA NDEGE

__________

__________

Marubani wa kutoka nchi tofauti duniani walikutana jijini London katika mashindano ya kufanya manuva ya ndege. London ndiyo mara ya kwanza inaukaribisha mchezo huo ambao umeshawahi kukaribishwa katika miji mikubwa duniani ikiwemo Abu Dhabi, U.A.E. Michezo hiyo ya kutafuta mshindi wake yalifanyika Jumamosi, tarehe 29/07/2007, Docklands, East London. Mchezo huo ulihudhuriwa na watu maarufu tofauti akiwamo Ex Waziri Mkuu wa U.K., Bwana Tony Blair na Mkewe Cherie Blair. Mashindano hayo hudhaminiwa na kinywaji maarufu duniani Red Bull, na jina la michezo hiyo inaitwa, Red Bull Air Race World Series. Mji wa pili kufanyika mashindano hayo utakuwa Budapest, Hungary, tarehe 19 na tarehe 20/08/2007.

__________

IRAQ YASHINDA KOMBE LA ASIA

__________

__________

__________

__________

__________

Kapteni wa timu ya Iraq, Younis Mahmoud pichani hapo juu akinyanyua kombe huku akishangilia ushindi baada ya kuishinda timu ya Saudi Arabia 1-0 katika fainali ya mashindano ya kombe la Asia lililofanyika huko Jakarta, Indonesia, tarehe 29/07/2007. Kapteni Younis alijipatia goli hilo katika dakika ya 71 baada ya kuusindikiza mpira golini kwa kichwa. Hilo ndilo kombe lao la kwanza Iraq katika mashindano ya kombe la Asia.


TAREHE 30/07/2007

UTANUZI WA BARABARA YA KILWA ROAD

Kilwa Road karibu na Polisi Ufundi

__________

Utanuzi wa barabara ya Kilwa Road ukiendelea sehemu mbalimbali za barabara hiyo

__________

Ujenzi unaendelea katika sehemu hii ya Mivinjeni ambayo ipo katika barabara ya Kilwa Road. Ujenzi huo ambao mpango wake ni utanuzi wa barabara na kupitisha mabomba ya maji na waya za umeme chini ya ardhi


TAREHE 31/07/2007

TANZANIA YATAFUTA MISS TANZANIA 2007

Mashindano ya Miss Tanzania 2007 yatafanyika Septemba mosi mwaka huu (1st September 2007) huko Dar es Salaam. Mashindano hayo yatamvua taji la umalkiwa wa Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, picha yake hapo juu na kuvikwa malkia mpya atakayepatikana katika mashindano hayo. Mashindano hayo yametayarishwa kwa kumwandaa mshindi atakayepatikana wa Miss Tanzania 2007, kushiriki katika mashindano ya dunia ya mwaka huu ambayo yatafanyika China, tarehe mosi Disemba (1st December 2007).

__________

Hawa ndio washindani wa mwaka huu 2007 wa Miss Tanzania, ambao mmoja wao anategemewa kuwa Miss Tanzania 2007.

__________

Gari ya stesheni ya redio ya Clouds FM ambayo imefungwa na mitambo ya kurusha habari zake moja kwa moja au (Live). Gari hiyo hutumika kwenda kwenye matukio mbalimbali na kuwaletea wasikilizaji wake habari motomoto moja kwa moja pale yanapotokea.


TAREHE 01/08/2007

JUU-CHINI, CHINI-JUU

__________

__________

Sio kimbunga! ndivyo ilivyojengwa. Nyumba iliyojengwa juu chini, chini juu katika kijiji cha Szymbark, Poland na msanii ujenzi, Bwana Daniel Czapiewski, ni nyumba moja wapo ya ajabu ya kiini macho ambacho hushangaza watalii kuona kuwa hata mapazia yako juu chini, chini juu.


TAREHE 02/08/2007

DARAJA LAVUNJIKA MJINI MINNEAPOLIS - MAREKANI

__________

__________

__________

__________

Daraja linalopita maji ya mto wa Mississippi liilopo mjini Minneapolis, huko Marekani, lilivunjika na kujeruhi na kuua baadhi ya watu. Daraja hilo lilivunjika wakati wa jioni wa saa za harakati za magari na watu waendao kwa miguu. Ajali hiyo imesababisha kusimamisha harakati hizo ambazo zimewafanya watu wa upande mwingine wa mto wa Mississippi wasiweze kuvuka kivuko hicho. Kutokana na waandishi wa habari, basi lililobeba jumla ya watu hamsini na tisa (59) wakiwamo watoto wa shule na watu wazima, liliweza kusimama futi chache tu kutoka kwenye daraja hilo wakati linapovunjika na kusalimika kuanguka kwenye mto huo.

__________

JELA YA PHILIPPINES YAKULETEA - THRILLER

__________

__________

__________

Jela ya wafungwa wa kisiwa cha Cebu kiliopo Philippines kimeanzisha program ya wafungwa wake kufanya mazoezi ya kucheza nyimbo kila asubuhi. Program hiyo imeanzishwa na mshauri wa ulinzi wa jela hiyo, Bwana Byron Garcia, ambaye amesema kuwa mazoezi hayo yatakuwa kama ni mazoezi ya viungo na kuwafanya wachangamke wakiwamo katika jela hiyo. Kila asubuhi wafungwa hao wanavaa nguo zao za kucheza na kufuatisha wimbo maarufu wa Michael Jackson, Thriller. Inavyosemekana wafungwa hao wapo katika maandalizi ya kufanya mazoezi ya kucheza nyimbo nyingine maarufu ya Vanilla Ice, Ice Ice Baby. Mazoezi hayo yamerushwa kwenye mtandao wa You Tube ambayo yametazamwa na watu zaidi ya milioni tatu kutoka pande tofauti duniani.


TAREHE 03/08/2007

KAMPALA - UGANDA

Hiki ndicho kituo kikuu cha teksi cha mjini Kampala, Uganda. Hapa daladala linaitwa teksi na teksi inaitwa spesho

__________

Hii ndio High Street ya Kampala. Safisha safisha macho hapo, juu kulia kushoto chini. Wasikwambie hujafika

__________

TAMASHA LA DUNIA LA KUSHEREHEKEA MAPUTO YA KUPAA

__________

 

Tamasha la dunia la kusherehekea maputo ya kupaa, lilivutia washiriki karibu thamanini (80) kutoka nchi tofauti duniani ambalo lilifanyika ufaransa (France). Tamasha hilo linatarajiwa kuvunja rekodi kwa kupaisha maputo ya kupaa mia nne (400) kwa wakati mmoja. Tamasha hilo linategemewa kuisha tarehe 05/08/2007.

__________

 GARI LA KUPAA

__________

__________

Kampuni ya Moller International U.S.A., wamezindua rasmi gari za kupaa hewani ambazo jina lake ni M200G. Gari hizo zinapaa juu kwa umbali wa mita tatu kutoka usawa wa ardhi, ni umbali kiasi cha kuipita gari nyingine ndogo ya kawaida. Gari hizo zipo katika majaribio na zikipasishwa zinategemewa kuuzwa £44,000 (paundi elfu arubaini na nne za U.K.).


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk