Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

TAREHE 11/08/2007

KWA VIJITI VYA MENO PIA?

__________

__________

__________

Mchoraji maarufu wa kutoka Albania, ameonyesha usanii wake wa uchoraji kuwa ana kipaji cha uchoraji si kwa kutumia rangi tu, anaweza kuchora picha hata kwa vijiti vya meno na kuifanya picha hiyo ionekane katika pembe tatu au (3D). Msanii huyo, Bwana Saimir Strati (41), ambaye anategemewa kuingia katika (Guinness Book of Records), au kitabu cha dunia cha kuvunja rekodi kwa uchoraji wake huo ambaye hajawahi mtu kuchora picha kubwa ya namna hiyo ya kuonekana katika pembe tatu kwa kutumia vijiti vya meno.

Bwana Saimir, anatumia vijiti vya meno milioni moja kuichora picha hiyo kwenye ubao maalum wa (polystyrene) ambao una saizi ya mita 8 (nane) za mraba. Kazi hiyo imekadiriwa kumalizika baada ya siku 25 katika mji mkuu wa Albania, Tirana.

__________

WA TANZANIA WA UTURUKI

Wa Tanzania wa Uturuki


TAREHE 12/08/2007

MHESHIMIWA LOWASSA AMPA POLE MHESHIMIWA MWAKANJUKI

Waziri Mkuu wa Tanzania, Bwana Lowassa, alimtembelea kumpa pole Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi wa Zenjy, Brigedia Jenerali Adam Mwakanjuki, ambaye alilazwa hospitali ya Muhimbili baada ya kupata ajali ya gari ambayo ilitokea wiki iliyopita. Ndugu na familia ya mheshimiwa Mwakanjuki, wametoa habari kuwa hali ya mheshimiwa inaendelea vizuri kabisa na atarudi katika hali yake ya kawaida muda si mrefu, Mungu akipenda.


TAREHE 12/08/2007

MBIO ZA MBUZI - DAR ES SALAAM

__________

__________

Hapo juu ni mashindano ya mbuzi ambayo hutokea kila mwaka katika mwezi wa nane. Madhumuni yake ni kukusanya pesa za kusaidia watoto walemavu, ujenzi wa madarasa na kadhalika. Mchezo huo ambao chanzo chake ni Uganda umeanzishwa Tanzania tangu mwaka 2001 kwa madhumuni hayo na kushirikisha washindani tofauti wa mbio za mbuzi. Hapo juu kama uonavyo ni mshindi wa mwaka huu wa mbio za mbuzi namba 10 (kumi) akiwa na wadhamini wake akiwamo bosi wa Holiday Inn, Bwana Adam Fuller.


TAREHE 13/08/2007

DARHATTAN YETU

Pichani hapo juu siyo Manhattan ni Darhattan yetu ionekanavyo hivi sasa, tumekosa (statue of Liberty) tu!


BASI LA MATANUZI

__________

__________

__________

__________

Mie sina la kusema!


TAREHE 14/08/2007

MHESHIMIWA JAKAYA KIKWETE NA RAIS WA MSUMBIJI

Rais wa Msumbiji, Bwana Armando Gwebuza akikaribishwa hivi majuzi nchini Tanzania na mwenyeji wake Rais wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Kikwete.

__________

Hapo juu pichani, ni uwanja ambao timu ya taifa ya Tanzania itacheza na timu ya taifa ya Msumbiji tarehe 08/09/2007.


TAREHE 15/08/2007

MASANJA MKANDAMIZAJI

Juu kushoto ni msanii mchekeshaji ambaye anachipukia kwa kasi huko Bongo katika wachekeshaji wanaotamba hivi sasa wakiwamo na akina Kingwendu, Mzee Small na Majuto. Msanii huyo ambaye umaarufu wake anajulikana kwa jina la Masanja Mkandamizaji amejipatia umaarufu wake kwenye filamu za kuchekesha na katika vipindi vya TV vinavyoitwa 'Ze Comedy'. Hapo juu, akijifurahisha na msanii mwenziwe, Mwanafalsafa.

__________

DAVID BECKHAM AJIPATIA GOLI LAKE LA KWANZA

__________

__________

David Bechkham (32), ajipatia goli lake la kwanza tangu ahamie Marekani, alipochezea timu yake, LA Galaxy. Timu hiyo ambayo ilipambana na timu ya DC United katika semi-fainali ya kugombea ushindi wa SuperLiga ya Marekani, David Beckham alijipatia goli lake katika dakika ya 28 alipopiga (free-kick) ya mtindo uliompatia umaarufu katika mchezo wa mpira wa miguu na kumuacha hoi! goli kipa wa DC United, Troy Perkins. LA Galaxy walishinda mabao 2-0.

Kwa ushindi huo, LA Galaxy wameingia fainali ambapo watapambana na wapinzani wao CF Pachuca, ambao waliwashinda Houston Dynamo katika kuingia fainali hiyo. Fainali itakuwa tarehe 29/08/2007.

 


TAREHE 16/08/2007

CHANDARUA ZA MBU

__________

Treni ambayo ipo Jamhuri ya Congo, imetumiwa kubebea vyandarua ambavyo vimetolewa kwa msaada. Msaada huo mpango wake ni kuwa mpaka mwisho wa mwaka huu, kila mwanamke mwenye mimba na ambaye ana mtoto wa chini ya miaka mitano nchini Jamhuri ya Congo, kupata chandarua. Kampeni hiyo ni katika kupigana vita na ugonjwa wa malaria ambao unaua wengi nchini Afrika, ambao unasababishwa na mbu.


PERU YAPATA MTETEMEKO WA ARDHI

__________

__________

__________

Lima imepata mtetemeko wa ardhi ambao umeacha maelfu bila ya makazi na kuua zaidi ya watu mia tano na kujeruhi zaidi ya watu elfu moja mia tano. Kabla ya mtetemeko huo, nchi nzima ilipewa tahadhari ya kimbunga cha Tsunami, lakini baadaye ikaghairishwa na badala yake wakaja kupata mtetemeko wa ardhi ambao wameukadiria athari yake haukuwa kama wangepatikana na Tsunami.

Rais wa Peru, Bwana Alan Garcia, alitoa amri katika vyombo vyake vya serikali kuangalia usalama na amani ya watu, utulivu na utovu wa nidhamu kwa wananchi wote ambao watakao kuwa mitaani kutokana na kuvunjwa kwa majumba yao.

__________

TAIFA STARS NDANI YA DENMARK

Timu ya Taifa Stars wakiwa ndani ya Denmark katika mechi za kirafiki

__________

DIAMOND JUBILEE HALL - DAR ES SALAAM

Diamond Jubilee Hall ilivyo sasa Dar es Salaam, ambayo mwaka huu 2007 inasheherekea kutimiza miaka 50 ya uongozi wa kiongozi wake Aga Khan kuanzia mwaka 1957 - 2007


TAREHE 17/08/2007

VIJANA WA TIMU YA ZENJYDAR

Watoto/vijana wa timu ya Zenjydar wakijiandaa kwa mechi za timu ya watano-watano, kwa kufanya mazoezi ya kuwakilisha 'Community' yao. Vilevile mazoezi hayo yatawasaidia kukutana na kujuana na vijana wenzao katika mambo ya maendeleo yao ya kijamii na ya kiafya. Pichani nyuma kushoto ni kocha wao, Bwana Ali akiwa na Mwenyekiti wa Zenjydar aliyevalia jezi ya timu ya taifa ya Tanzania, Bwana Saleh Jaber.

__________

Mazoezi ya viungo

Mazoezi ya kupiga mpira na 'control'

Mpira uwanjani

'Team work'

Ustadi uwanjani

Hatari golini

Stamina na ustadi


- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk