|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
TAREHE 25/08/2007 WAZIRI WA AFYA WA MAREKANI AITEMBELEA ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la mapinduzi, Mheshimiwa Amani Abeid Karume akiongea na Waziri wa Afya wa Marekani, Mheshimiwa Michael Leavitts, huko Ikulu, Zenj. TAREHE 26/08/2007 USANII WA UCHORAJI WA PEMBE TATU AU (3D)
__________
__________
Picha zote tatu uzionazo hapo juu ni picha za kuchora. Wasanii wanazidi kuendeleza vipaji vyao katika uchoraji wa mabodi ya magari katika mtindo wa (three dimension) au picha kuonekana kwa pembe tatu. __________ TIMU YA WATANZANIA WA SWEDEN
__________
Uzinduzi rasmi wa timu ya FC Kilimanjaro ya wa Tanzania waliopo Sweden, ilifunguliwa na mgeni rasmi ambaye ni katibu mkuu wa wizara ya habari, utamaduni na michezo wa Zenj, Dk. Omar Shajak, akiwa na kaimu msaidizi wa balozi wa nchi za Skandinavia, Mheshimiwa Jacob Msekwa, huko huko Sweden. __________ TAIFA STARS WAKIWA NDANI YA USWIZI
__________
__________
Taifa stars (timu ya taifa ya Tanzania) walimtembelea balozi wa Tanzania aliyopo Uswizi, Mheshimiwa Marten Lumbanga, katika ziara nchini Uswisi. Pichani juu, balozi akionekana kasimama pembeni ya kiongozi wa msafara na makamu wa mwenyekiti wa TFF, Bwana Jamal Bayser, na kocha wa Taifa stars, Bwana Maximo. Taifa stars walishinda bao 1-0 dhidi ya timu ya Kuwait katika mechi iliyofanyika huko-huko Sweden, tarehe 25/08/2007. Taifa stars wanajiandaa na pambano lao na timu ya taifa ya Msumbiji litakalofanyika tarehe 08/09/2007. __________ SIYO PANCHA! NI MAPOZZZ!!!
Siyo pancha, hiyo ndio gari maarufu iitwayo Hummer. Gari hizo huja katika kila shepu ya muundo (pesa zako tu!) na moja wapo ndio hio hapo pichani juu. TAREHE 27/08/2007 MKONO WA POLE
Kamishna mkuu wa magereza, afande Nanyaro (kulia) akipewa pole na mkuu wa majeshi, Jenerali George Waitara baada ya mazishi ya mkewe (Mama Nanyaro) katika makaburi ya Kinondoni, Dar es Salaam. Wengine kushoto ni afande Tibaigana na inspekta jenerali wa polisi mstaafu afande Omar Mahita. __________ HAYATI SHEIKH NURDIN
Masheikh wa msikiti wa Shadhly na wakubwa kutoka serikalini wakionekana pichani wakimswalia sala ya maiti, hayati Sheikh Nurdin Hussein aliyefariki Jumamosi katika hospitali ya Tumaini, Dar es Salaam, na maiti ilisafirishwa na kuzikwa huko Kilwa siku ya Jumatatu, tarehe 27/08/2007. Pichani wakiwemo Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Ali Shein katika sala ya maiti msikiti wa Shadhly. TAREHE 28/08/2007 KAMPENI YA KUWAPA MOYO TAIFA STARS
Naibu waziri wa habari utamaduni na michezo Mheshimiwa Joel Bendera, akizindua kampeni ya kupiga sahihi ya kuiunga mkono timu ya taifa stars katika uwanja wa Karume. Kampeni hiyo ni katika kuwahimiza wananchi waishangilie timu yao itakapocheza na timu ya taifa ya Msumbiji. __________
Kitwana Manara ambaye sasa ni diwani wa Buguruni akitia sahihi yake katika kushadidia kampeni hiyo. __________
Washabik wakishangilia kampeni ya kuwaunga mkono Taifa Stars wakiwepo hapo uwanja wa Karume, Dar es Salaam. __________ BODA KWA BODA NDANI YA TANGA
Hili ni jengo la bandari ya Tanga lililopo katika barabara ya bandari. __________
Jengo la Nasaco ambalo lipo mkabala na jengo la bandari ya Tanga katika barabara ya bandari. TAREHE 29/08/2007 OSCAR KAMBONA
Hapo juu pichani ni Oscar Kambona. Ndiye mtu wa kwanza kutangaza Kiswahili katika idhaa ya Kiswahili BBC London tarehe 27/06/1957. Alifariki huku-huku England akiwa na umri wa miaka 68. TAREHE 30/08/2007 DA LA DA LA AU PI KI PI KI?
Hapo juu pichani ni mtaa wa Azikiwe, Dar es Salaam ionekanavyo hivi sasa. Kondakta aonekana akijaribu kumvutia pembeni mwenye pikipiki ili waweze kumaliziana kabla ya wajomba hawajafika. __________ 31/08/2007 WANJA LETU LA TAIFA - BY NIGHT
__________
Huu ndio uwanja wetu mpya wa taifa uonekanavyo usiku mjini Dar es Salaam __________ SHULE YA WINGWI
Aisha Issa (kushoto) na Bi Kombo Bakari wakisoma utenzi kwa Rais wa Zanzibar, Mheshimiwa Amani Abeid Karume katika ufunguzi wa madarasa mapya ya skuli ya Wingwi iliyopo huko Zanzibar. __________ USANII WA UCHORAJI - KARIBU KAHAWA
[photogallery/photo00025538/real.htm]
- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|