|
Zenjydar Community Association H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE È 07886 535282
|
|
|
Miss Zhang Zilin (23) wa China, kavikwa taji la Miss world 2007 huko Sanya ambapo ni kitovu kikubwa cha utalii ambacho kipo katika kisiwa cha Hainan kusini mwa China. Ni mara ya kwanza China kushinda Miss world ambayo imwewakilishwa na Miss Zhang ambaye alikuwa ni sekretari katika mji wa Beijing. Wa pili badala yake alifuatia Miss Angola, Micaela Reis na kufuatiwa na mshindi wa tatu Miss Mexico, Carolina Moran Gordillo.
Miss Tanzania akiwa na rafiki yake Miss Trinidad & Tobago
Miss Tanzania akiwa amejichanganya na rafiki zake katika ukuta mkubwa wa China
Mheshimiwa Nelson Mandela alitoa hotuba yake juu ya Miss world 2007 na World Aids day ambayo ni tarehe 1 Disemba
Kama uonavyo hapo juu, ni vurumai baina ya wamachinga na askari wa jiji. Siku nyingi tu tangu serikali ipige marufuku wamachinga kuuza bidhaa zao ndogondog katikati ya mji bila ya mpango. Wamachinga hawakuafikiana na hayo na bado wanaendelea kuuza vitu vyao mitaani bila ya ruhusa. Kwahiyo, kuanzia mtaa wa Congo mpaka mtaa wa Jamhuri askari wa jiji walikuwa na kazi moja tu! pigapiga. Kama uonavyo, wengine wakicheza kavu kavu na askari wa jiji na wengine chini wakitoka mbio kujiepusha na virungu.
JK akimsindikiza
mkewe Mama Salma Kikwete katika uwanja wa ndege wa
Tabora jana ambapo mama Salma alielekea Mwanza
kuhudhuria tamasha la vijana kupinga ukimwi kama
mgeni rasmi na Rais Kikwete kubaki Tabora ambapo
maadhimisho ya siku ya ukimwi duniani yalifanyika
kitaifa mkoani humo.
Akiwahutubia vijana
katika uwanja CCM Kirumba huko Mwanza, Mama Kikwete
aliwaasa vijana hususan wanafunzi wa kike kuvikataa
vishawishi vya fedha na zawadi kutoka kwa watu
wanaotaka kuwarubuni kimapenzi na alitoa wito kwa
viongozi wa serikali na mashirika ya umma kuimarisha
kampeni ya upimaji na ushauri.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Amani Abeid Karume, akipewa maelezo na msemaji wa Shirika la PSI hapa Zanzibar bwana Mshamu, wakati alipotembelea maonesho hayo katika banda la shirika hilo, linalotoa elimu ya kujikinga na maambukizi ya VVU (virusi vya ukimwi), katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yaliyofanyika jana, Machui Mkoa wa Kusini Unguja. Kulia ni mke wa Rais, Mama Shadya Karume.
Wakazi wa kutoka sehemu tofauti walihudhuria kuadhimisha siku ya ukimwi duniani
Dk. Ali Shein akisalimiana na Mheshimiwa Seif Sharif walipokutana katika lonji ya VIP ya kiwanja cha ndege Dar es salaam
RAIS wa Zanzibar pia ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa Suza, Mhe Amani Abeid Karume, akizungumza na wahitimu wa mahafali ya 3 ya Chuo hicho wa Shahada na Stashahada na Vyeti jumla ya wanafunzi 156, wakiwemo Shahada ya sayansi na Elimu, Stashahada Lugha na Elimu na Shahada ya Sanaa na Elimu, pia fani ya Sayansi ya Kompyuta na Teknolojia ya Habari.katika viwanja vya Victoria Garden.
Picha kwa hisani ya Ramadhan Othman Ikulu Zanzibar
RAIS wa Zanzibar, Mhe. Amani Abeid Karume, akisalimiana na wanafunzi katika ufunguzi wa skuli mpya ya Kisiwani Mkoa wa kaskazini Pemba, wakati alipofanya ziara ya Mikoa ya Pemba.
Tangu mwaka 1964, Australia walianzisha kuunda vitu vya matumizi ya kawaida kwa mwanadamu kuvifanya katika muundo mkubwa ikiwa kama ni moja ya mapambo ya kupendezesha nchi yao. Hapo juu ni 'The Big Banana'.
The Big Chook
The Big Macadamia Nut
The Big Boxing Crocodile
The Big Cow
The Giant Goldpanner
Big Golden Guitar
The Big Oyster
The Big Pineapple
The Big Shrimp
Cheka na vikatuni
Kuepuka kodi - Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com - - Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran! |
|
|
|