Zenjydar Community Association

H Harold Centre, 170 Harold Road, Plaistow, London, E13 0SE

È 07886 535282

? zenjydar@gmail.com

 

WIKI ILIYOPITA KWA UFUPI

08/12/2007

ANDREW BUTLER & CHRISTOPHER AVERY

Andrew Butler na Christopher Avery ni vijana wanaoishi Ohio, USA, ambao kwa sasa wanatarajia kifungo cha miaka 20 jela kwa kuingilia benki ya mjini Ohio na kuiba pesa. Kabla ya kuingia katika benki ambayo picha zinaonekana hapa. Vijana hao waliingia katika benki nyingine siku moja kabla ya siku hii na kujaribu kuiba pesa lakini hawakufanikiwa na waliweza kukimbia bila ya kukamatwa. Siku hii ambayo picha zake zimechukuliwa waliweza kuiba pesa za dola ambazo zina thamani ya £63,000 (elfu sitini na tatu). Kutokana na juhudi za polisi wa marekani na ushahidi uliokuwepo, vijana hao wawili walikamatwa na kuhukumiwa mahakamani. Walipoulizwa kwanini walitaka kuiba pesa hizo, walisema kuwa tulihitaji pesa kwasababu ya fii za kulipia chuo kikuu. Wote wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 20 badala ya miaka 108 ambayo wanapaswa kuhukumiwa.

Andrew Butler (kushoto) na Christopher Avery (kulia)


09/12/2007

MIAKA 46 YA UHURU

Gwaride likipiga kwato katika maonyesho ya Uhuru katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma, Tanzania

Mvua kubwa ilinyesha na kuchafua jeshi la ulinzi na usalama wa Tanzania, lakini maonyesho yaliendelea

Halaiki ya watoto walipendeza huku wakiimba "Tanzania, Tanzania, nakupenda kwa moyo woooteeeee..."

Amiri jeshi mkuu wa majeshi ya ulinzi na usalama, rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika maadhmisho ya uhuru wa Tanganyika, akiwa na mkuu wa majeshi ya ulinzi, jenerali Davies Mwamunyange.

Ngoma mbalimbali zilitumbuiza katika siku ya Uhuru mjini Dodoma ikiwemo ngoma ya Msewe

Wakubwa wa nchi walihudhuria kuadhimisha sikukuu ya miaka 46 ya uhuru katika uwanja wa Jamhuri, Dodoma

Balozi wa Tanzania nchini UK, Bi Mwanaidi Maajar (kulia) akiwa na mumewe Mh. Sharif Maajar wakiwa katika sherehe za kuadhimisha miaka 46 ya uhuru katika uwanja wa Wembley, mjini London.


10/12/2007

TAARAB YAZIDI UMAARUFU

Umashuhuri wa taarab wazidi kupanda Dar es salaam

MAFIA AIRPORT - TANZANIA

Ndege imetua katika uwanja wa ndege wa kisiwa cha Mafia, Tanzania

Uwanja wa ndege wa Mafia, Tanzania


11/12/2007

KIAPO

Jk akimwapisha balozi Anthony Itatiro kuwa Mkurugenzi wa Itifaki ikulu jijini Dar es salaam. Itatiro anachukua nafasi ya balozi Cisco Mtiro aliyeteuliwa kuwa balozi wetu huko Malaysia. Vilevile, JK ameondoka usiku wake kuelekea Washington DC ambako keshokutwa desembe 13 atakuwa na hafla ya mfuko wa Leon H. Sullivan ambapo atatumia fursa hiyo kuwaalika rasmi wafanyabiashara na wengine kuhudhuria mkutano utakaofanyika mwanzoni mwa mwezi Juni mwakani huko Arusha.

Rais Jakaya Kikwete akimwapisha balozi Alex Masinda kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Asia katika Wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa huko ikulu Dar.


12/12/2007

MZINGA

Basi la upendo toka Dar kwenda Mbeya lilipata mzinga (ajali) jana mchana sehemu za Mafinga, Iringa, baada ya kulivaa roli la tela lilokuwa limeegeshwa pembeni. Watu kadhaa walijeruhiwa.

MAHUJAJI

Mama Salma Kikwete akiongea na kuwafariji mahujaji waliokwama uwanja wa ndege Dar es salaam kwa siku kadhaa ambayo ilimfanya mpaka rais JK aingilie kati na kutatua tatizo hilo la kusafirisha mahujaji walioondoka mwaka huu.


13/12/2007

MANDHARI YA DAR

Mandhari ya Dar es salaam inazidi kubadilika kuwa ya kuvutia

KUENDESHA GARI NA ULEVI HAVIENDI SAMBAMBA

Katika kampeni ya serikali kupigana vita na 'drink and drive', wameweka glasi kubwa ya bia katikati ya stesheni ya treni ya Paddington, London, ndani yake amewekwa mtu ambaye amejitolea kukaa ndani ya glasi hiyo, ambaye ameshawahi kukamatwa akiendesha gari na hali ya kuwa amelewa katika siku za nyuma.


14/12/2007

NDO NDI AU DING DONG

Bondia Ricky Hatton amewasili UK baada ya kutoka Las Vegas kwenye mashindano ya ngumi baina yake na Floyd Mayweather wa Marekani, ya kugombea ubingwa wa Welterweight wa dunia yaliyofanyika Jumamosi ya tarehe 8/12/2007. Ricky alipotua tu katika uwanja wa ndege wa Manchester, alipokelewa na 'girlfriend' wake Jennifer Dooley na akatangazia vyombo vya habari kuwa anatarajia kupigana tena na Floyd kwa mara ya pili. Ricky alipigwa na kuangushwa katika raundi ya kumi na ushindi ukaenda kwa Floyd Mayweather. Lakini baada ya ngumi hizo na baada ya kupigana kwa maneno kwa siku kadhaa kabla ya kukutana ulingoni, mwishowe walikumbatiana kirafiki na kukumbushana kuwa huu ni mchezo tu.

Mayweather (kulia) na Hatton (kushoto)

CAPELLO KOCHA MPYA WA ENGLAND

Imetangazwa rasmi kuwa Fabio Capello (61) wa Italy kuwa meneja mpya wa England. Capello ameshasaini 'contract' yake na FA (Football Association) ya miaka minne na nusu ambayo itaanza January 7, 2008.


KATUNI

Cheka na vikatuni

HII SIO KATUNI

Hasira za Liverpool kufungwa!


- Tutumie picha na habari tofauti za kutoka popote na tutaziweka kwenye mtandao - Email: zenjydar@gmail.com -

- Picha za Bongo na Issa Michuzi - Shukran!

© www.zenjydar.co.uk